SALAMU ZA AYATULLAH SAYYID ALI KHAMANEI (2001).

 Amirul-Muuminiin Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni kiigizo kilichokamilika kwa watu wote, ujana wake ulikuwa ni nguvu yenye ushujaa nacho ni kiigizo kwa kila kijana. Serikali yake yenye uadilifu na usawa ni mfano mwema kwa dola (Serikali) nyenginezo. Hapana shaka kwamba maisha yake yote katika jihadi na majukumu aliyokuwa nayo ni mfano bora kwa Waumini wote, uhuru aliokuwa nao ni mfano mwema kwa wapenda uhuru kote ulimwenguni, naam, mazungumzo yake yaliyojaa hekima na mafunzo yake ya milele ni mambo ya kuigwa na wasomi na wanataaluma wote.