BOKO HARAM WAENDELEZA UKATILI NIGERIA.

Magadi wa kundi la Kitakfiri la Boko Haram wameuteka tena mji ulioko mpakani wa Marte kaskazini mwa Nigeria. Gavana na jimbo la Borno anasema kuwa magaidi hao wameudhibiti kabisa mji huo na kusema kuwa hilo ni pigo kubwa kwa jeshi la Nigeria. Mji huo wenye umuhimu mkubwa kiuchumi kwa eneo la kaskazini mwa Nigeria uko katikati ya njia ya kibiashara inayotoka Cameroon na Chad. Marte umebadilisha utawala kutoka kwa majeshi ya serikali na magaidi wa Boko Haram mara kadha tokea mwaka wa 2013 hadi sasa. Wakati huo huo watu saba walipoteza maisha jana baada ya msichana mdogo aliyekuwa amejifunga mabomu mwilini kujilipua mjini Damaturu katika jimbo la Yobe kaskazini mwa Nigeria. Watu wengine 31 wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliojiri ndani ya kituo cha basi. Maafisa wa usalama wanasema msichana aliyetekeleza hujuma hiyo alikuwa na umri wa miaka 12. Kwingineko imearifiwa kuwa magaidi wa Boko Haram wanatoa mafunzo kwa wasichana 600 ili watekeleze hujuma za kulipua mabomu kwa kujitoa muhanga katika mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri. Naibu Gavana wa jimbo hilo Alhaj Zannah Mustapha amesema ili kukabiliana na hali hiyo sheria za kutotoka nje zitaendelea kutekeleza katika jimbo hilo. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/48833-boko-haram-waendeleza-ukat…