NASRALLAH: MATAKFIRI NI NJAMA YA MAREKANI NA WAZAYUNI.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Lebanon, Hizbullah, amesema kuibuka Matakfiri ni katika njama za Marekani na Wazayuni.
Akizungumza kwa njia ya moja kwa moja kupitia Televisheni siku ya Jumamosi, Sayyid Hassan Nasrallah amesema Matakfiri wa Lebanon, Syria na Iraq wameunda Nakba au maafa mapya na hivyo ametoa wito wa kuwepo jitihada za kukabiliana na mradi huo wa Marekani na Wazayuni.
Inafaa kuashiria hapa kuwa Matakfiri ambao aghalabu ni Mawahabi humkufurisha kila Mwislamu asiyekubaliana na itikadi zao potofu.
Sayyid Nasrallah ameashiria ushindi wa hivi karibuni wa Hizbullah na Jeshi la Syria katika eneo la Qalamoun na kusema kulikuwa na mapambano makali juu ya milima na mabondeni. Kiongozi wa Hizbullah amesema Matakfiri wamelazimika kurudi nyuma baada ya kupata pigo kubwa na kuongoza kuwa, mapignao bado yanaendelea. Amesema hivi sasa wapiganaji wa Hizbullah wamekata njia za Lebanon zilizokuwa zikitumiwa kuwafikisha misaada magaidi nchini Syria. Aidha amepinga madai ya vyombo vya habari kuhusu idadi ya waliopoteza maisha miongoni mwa wapiganaji wa Hizbullah katika oparesheni za Qalamoun na kusema ni wapiganaji 13 tu wa harakati hiyo ndio waliokufa shahidi katika oparesheni hizo.