Uislamu ni shule ya itikadi ya Kifo cha kishahidi na hususani sura ya
kweli ya Uislamu ambayo inaitwa Ushia ni mtoto wa Kifo cha Kishahidi.
Ushia ni shule ambayo imelelewa katika mapaja ya Kifo cha kishahidi na
ni matokeo ya Kifo cha kishahidi. Shule hii imegeuzwa kutoka njia ambayo
Maimamu Maasumin (a.s) wa Ushia walivyofundisha na kuwasilishwa baada
ya kuingia katika mikono isiyo na uwezo; waliugeuza Ushia kuwa kitu
tofauti kabisa. Dini ya Mashahidi wakati inapoingia katika
mikono ya watu waoga, hawajitengi tu kutokana na kujifunza ujasiri na
ushujaa kutoka kwenye shule hii lakini badala yake hugeuka kuwa dini ya
waoga. Na inatajwa katika hadithi kwamba hutakiwi kamwe hata kusafiri
pamoja na waoga na hata kukaa karibu nao, ili kwamba usipate athari za
uwoga wao. Imesemwa kwamba kamwe usitake ushauri kutoka kwa waoga katika
suala lolote, wala hata msiwaozeshe mabinti zenu kwa waoga. Kwanza
tunauliza kama mvulana ana kipato kizuri au la. Kwanza lazima tuulize
kama ana akili au la, na kama ana akili chunguza je, sio muoga.
Amirul Muminin (a.s) alimuomba kaka yake ampatie mke kutoka familia ya
shujaa kwa sababu Ali (a.s) hataki mtoto wake yeyote kuwa muoga. Hili
hutuambia kwamba ni jukumu la akima mama kukuza ushujaa kwa watoto na ni
akina mama ambao ndio wanaolea ari ya Kifo cha kishahidi kwa watoto
wao. Mama sio yule anayeweka uso wa mtoto wake mara tu anaposikia Kifo,
bali badala yake wakati ambapo anamlisha maziwa lazima vilevile amlishe
asali ya Kifo cha kishahidi. Basi watoto hawa hujipatia hadhi fulani.
Kuna hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ambapo anataja maadili tofauti katika mpangilio ulio bora, ambamo maadili gani yako juu ya maadili mengine na mwishowe anasema kwamba kubwa mno ya maadili yote ni kufa Kifo cha kishahidi katika njia ya Allah; na hakuna maadili makubwa kama haya. Swali ni kwamba kwa nini haya ni maadili makubwa sana? Shahidi sio jina la sifa kwa ajili ya mwili uliokufa; ni jina la Falsafa ya maisha. Shahidi hutoa maisha yake kwa jumuiya; lakini kwenye jumuiya zile tu ambazo hukaa katika darasa la Shahidi na kujifundisha somo la maisha kutoka kwake. Shahidi sio mwenye kutegemea au kutamani Sura Fatiha. Shahidi wala hata haogopi kile kitakachomtokea kama akifa. Na Ustadh Sayyed Jawwad Naqvi