Sheikh
Hemedi Jalala Kiongozi wa Chuo cha dini ya Kiislam Kigogo Post, Dar es
Salaam, amekutana na viongozi wa Msikiti wa Mtambani uliyopo Kinondoni
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana juu ya changamoto
mbalimbali zinazowakumba waislamu ndani na Nje ya Nchi. Mazungumzo yana
lengo la kuwakutanisha viongozi wa dini tukufu ya Kiislamu katika meza
moja na kujaribu kutizama changamoto zinazoukabili uislamu ikiwemo
hatari ya Makundi ya kukufurishana na Ugaidi yanayokithiri kuibuka kila
uchao. Aidha mazungumzo yanalengo kutafuta njia za kuwaunganisha
Waislamu na kuwa na sauti moja katika masuala yanayowaunganisha dhidi ya
Maadui zao.