BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA YAFANYA UFUNGUZI WA MSIKITI KATIKA KIJIJI CHA BOMBO MAJI MOTO.

Leo mnamo tarehe 10/04/2015 sawa na mwezi 20 Jamad Thani, Taasisi ya Bilal Tanga,imefanya ufunguzi wa msikiti mpya katika kijiji cha Bombo maji moto baada ya waumini wa sehemu hiyo kuwa na tatizo la muda mrefu la kukosa msikiti wa kufanyia ibada zao.Kwa uwezo wa Allah (s.w),Taasisi hiyo ya Bilal baada ya kugundua tatizo hilo imeweza kufanya haraka na kujenga msikiti huo na leo hii kuwakabidhi waislam wa kijiji hicho.
Mwenyeezi Mungu (s.w) awazidishie wafadhili hao kila la kheri na baraka katika kazi zao.Inshallah.
Washukran.
Na Sheikh Taqee