Mkuu wa Shirika la Hija na Umra la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema
kuwa kuna uwezekano wa kufutwa safari zote za ndege za Wairani
wanaokwenda Saudia Arabia kwa ajili ya ibada ya Umra.
Hatua hiyo
imekuja baada ya askari wawili wa Saudia kuwadhalilisha kijinsia
mahujaji wawili vijana wa Kiirani katika uwanja wa ndege wa Jeddah
waliokuwa wakirejea nyumbani baada ya
kukamilisha ibada ya Umra. Kwa kutumia kisingizio cha kuwapekua vijana
hao, askari wawili wa Saudia walifikia hatua ya kutaka kuwanajisi lakini
mahujaji wenzao walichukua hatua za haraka za kutoa taarifa
zilizopelekea kukamatwa askari hao wawili.
Mkuu wa Shirika la Hija na Umra la Iran amemtaka Waziri wa Hija wa Saudia, Bandar bin Muhammad kuwafungulia mashtaka na kuwachukulia hatua kali askari hao wahalifu ili kurejesha imani na utulivu wa kiroho kwa mahujaji wa Iran wanaokwenda nchini humo kwa ajili ya ibada za Hija na Umra.