NIGERIA YAFANYA SHEREHE YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA MTOTO WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W).

Sherehe ya kukumbuka mazazi ya bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) Fatma Zahra (a.s) iliyofanyika katika nchi ya Nigeria.
Fatma Zahra (a.s) ni binti wa Nabii Mtukufu na ni mke wa Imam Mtukufu na ni mama wa wajukuu wawili Hassan na Hussein mabwana wa vijana wa Peponi. Hakika yeye ni uso wenye kung'ara kwa ajili ya Utume wa mwisho, na ni chombo safi kwa ajili ya kuendeleza kizazi kitakatifu, na ni chimbuko safi la kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) huku akiwa ni mbora wa Wanawake wote ulimwenguni.