CHUO CHA KIISLAMU CHAFANYA MUHADHARA WA AMANI.

Sheikh Hemed Jalala, Kiongozi wa Chuo cha Kiislamu kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam jirani na kituo kidogo cha Polisi amewataka Waislamu kufuatilia Uislamu halisi wa Mtume Muhammad(s.a.w) ambao ni Uislamu wa amani, huruma na maelewano amesema kuwa Uislamu halisi utashinda Uislam wa chinja chinja utafeli kwa kuwa unaenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu (s) aidha amewataka watu wote bila kujali dini zao kushikamana na kusikilizana kwani jamii ambayo aina maelewano itakuwa ipo mbali na maendeleo, taifa ambalo linapata maendeleo ni taifa lenye maelewano na mshikamano.
Katika Muhadhara huo uliyomalizika siku ya J.pili ya tarehe 1/03/2015 kulitolewa vitabu mbalimbali vinavyoonesha athari mbaya ya Madhehebu ya Kiwahhabi (ANSWARU SUNNA) Madhehebu ambayo hii leo yamekuwa tishio kubwa kwa jamii ya Kiislamu Ulimwenguni kwa maana watu hawa wamevaa vazi Tukufu la Uislamu na kufanya mauaji ya kikatili na kishenzi kwa kisingizio cha Uislamu hivyo kitabu hicho kimeweka wazi njama za Madhehebu hayo potofu na korofi pia kulifuatia na ugawaji wa Barua iliyoandikwa hivi karibuni na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei alitoa ujumbe kwa vijana wa nchi za Magharibi ambapo kati ya mengine amewataka wafanye uchunguzi kuhusiana na ukweli na taswira wanayopewa kuhusu Uislamu. Ujumbe huo umeendelea kuakisiwa kote duniani.