Baadhi ya Waumini wakiwa katika mazishi ya Mwanaharakati wa Madhehebu ya
Ahlul Bayt (a.s) Bi Subira aliyefariki siku ya J.tano na kuzikwa siku
ya Alhamisi tarehe 26/02/2015 katika kijiji cha Mtindilo Wilayani
Lushoto, katika mazishi hayo amehudhuria Sheikh Waziri Nyello aliyekuwa
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Ithna Ashariyyah Community (T.I.C).
Swala ya Jeneza iliongozwa na Sheikh Baqri Mwenda Imam wa Masjid Imam
Ali bin Abi Talib (a.s) Lushoto. "Hakika sisi sote ni waja wa Mwenyezi
Mungu na kwake tutarejea" Tusome Suratul Fatha kwa ajili ya ndugu yetu.