Watu wamekubali uvumilivu kwenye Ukandamizaji kama sifa nzuri na maadili mema, kama ambavyo muundo uliopotoshwa wa Ukristo ulivyoanzisha hili kama maadili ya heshima na kulihubiri hili katika mielekeo hii. Lakini somo ambalo Imam Hussein (a.s) amelitoa juu ya kutovumilia Ukandamizaji litabakia kuwa hai mpaka mwisho wa Ulimwengu huu, na kwa ubora wa hili yeye (a.s) ameonesha njia ya kutovumilia Ukandamizaji daima. Umma ulikuwa mvumilivu wa Ukandamizaji katika zama hizo na umekuwa na tabia ya kuzoea ukatili wa Bani Umayyah. Imam Hussein (a.s) alisema: "Napenda kuamrisha mema na kukataza maovu."
Nimekuja kuhuisha maadili na kutokomeza maovu. Uvumilivu kwenye Ukandamizaji ambao ni miongoni mwa maovu umekuwa sifa kwa watu katika wakati huo. Yeye (a.s) aliurekebisha Umma usiwe na uvumilivu kwenye Ukatili. Yazid ni Mkandamizaji lakini kamwe msiwe taifa la Yazid, hivyo mfuasi wa Hussein (a.s) ni mtu ambaye si Mkandamizaji na wala havumilii Ukandamizaji.
Katika siku ya Ashura wakati mtu mmoja kutoka jeshi la Umar ibn Saad alisema: "Kwa nini huli kiapo cha utii (kwa Yazid)? Kwa nini hunyenyekei kwenye utawala wa Bani Umayyah, kama utanyenyekea na kuwakubali kama watawala suala hili litakuwa limekwisha." Yeye (a.s) akajibu: "Kamwe sitatoa mikono yangu katika mikono yenu kwa udhalilifu na wala sitakimbia kama watumwa."
Rejea: Manakibe Ale Abi Talib, Juz. 4, uk. 18
Hapana shaka kwamba kulikwa na Ukandamizaji katika Karbala na watu wa Karbala walikandamizwa, lakini hatuoni uvumilivu kwenye Ukandamizaji. Uthibitisho muhimu kwa hili ni wale mashahidi na mateka, mtu yeyote ambaye hakubali Ukandamizaji anapata kifo cha kishahidi. Kifo chake cha kishahidi (a.s) na kuuawa kishahidi kwa watoto wake na masahaba wake kumethibitisha kwamba njia ya Imam Hussein (a.s) ni kupigana dhidi ya Ukandamizaji. Njia hii ni kuwa imara dhidi ya Wakandamizaji na kukataa Ukandamizaji wao na ukatili wao. Wale watu wakubwa walikuwepo wakati huo ambao hawakuuawa na hata upepo wenye joto wa Karbala haukuwagusa, hakuna aliyekwaruzana nao, kwa kweli walikuwa wanafurahia ibada yao na kutoa darasa zao, hii ni kwa sababu walikuwa wavumilivu wa Ukandamizaji.
Wakati mwingine washairi wetu husoma baadhi ya beti, ingawa beti hizi hazihubiri Ukandamizaji lakini zina masomo ya uvumilivu kwenye Ukandamizaji. Beti hizi lazima ziandikwe na kusomeka kama ambazo hazitoi masomo ya Ukandamizaji wala kukubali uvumilivu wa Ukandamizaji. Beti ambazo hutoa masomo ya Ushujaa, katika moyo na uadilifu lazima ziandikwe. Na Ustadh Sayyed Jawwad Naqvi