Sheikh
Abdul Rab Rasul Sayyaf, mmoja wa Maulamaa maarufu wa Kisuni wa nchini
Afghanistan amesema kuwa, kundi la kigaidi la Daesh ni adui wa
ubinadamu. Shirika la habari la Nasim limemnukuu Sheikh Sayyaf akisema
kuwa, kundi la Daesh linautumia vibaya Uislamu ili kufanikisha malengo
ya Marekani na utawala wa Kizayuni kwa lengo kuuangamiza Uislamu.
Ameongeza kuwa, jinai za kundi la Daesh katika eneo la Mashariki ya Kati
ikiwa ni pamoja na kumchoma moto akiwa
hai rubani wa Jordan, ni dhidi ya Uislamu na uanadamu. Sheikh huyo wa
Madhehebu ya Kisuni ameongeza kuwa, iwapo kundi la kitakfiri la Daesh
litajaribu kuingia Afghanistan, basi wananchi wa nchi hiyo watasimama
kidete kukabiliana nalo. Itakumbukwa kuwa, wakati kundi la kigaidi na
kibaath la Daesh lilipoundwa mwezi Oktoba 2006 baada ya kufanyika vikao
kadhaa baina ya makundi mbalimbali yenye silaha nchini Iraq, lilidai
kuwa limeundwa ili kuwatetea Masuni nchini Iraq, hata hivyo Waislamu wa
Kisuni ni miongoni mwa wahanga wakuu wa jinai za kundi hilo
lisilomvumilia yeyote ayanepinga fikra zake za kigaidi na za kukufurisha
Waislamu wengine.
TANZANIA YAKANUSHA KUWEPO AL SHABAB ENEO LA TANGA.
Afisa mwandamizi wa polisi nchini Tanzania amekanusha tetesi kuwa magaidi wa kundi la Al-Shabab wamekabiliana na vikosi vya usalama katika eneo la Tanga. Kamishna wa Oparesheni katika jeshi la Polisi CP Paul Chagonja amenukuliwa na vyombo vya habari akisema jana kuwa askari wawili wa jeshi la polisi na askari wanne wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ wamejeruhiwa vibaya kwa risasi baada ya kutokea mapigano kati yao na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika mapango ya Amboni mkoani Tanga.
Akitoa taarifa rasmi ya jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo jana Jumamosi, Chagonja amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Ijumaa ambapo amesema kuwa si tukio kubwa kama linavyoelezwa na baadhi ya watu na kwamba waliohusika ni majambazi na siyo magaidi. Amesema kilichotokea ni oparesheni ya kawaida iliyofanywa na jeshi la polisi kuwasaka watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliodaiwa kujificha katika mapango hayo na ndipo yalipotokea mapigano hayo yaliyoambatana na kurushiana risasi na kupelekea askari hao kujeruhiwa.
Amesema baada ya hali kuwa tete, jeshi hilo lililazimu kuomba msaada kutoka kwa askari wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ ambao walifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kutuliza hali ya taharuki iliyokuwa imetanda katika eneo hilo.