WAISLAM WAMETAKIWA KUKABILIANA NA MAADUI WANAOMPIGA VITA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).
Sheikh Sheikh Abdullatif Swaleh: Mtume (s.a.w.w) anapigwa vita na anafanyiwa uadui wa kila aina kutoka katika pande mbalimbali kuna pande ambazo zinazojinasibisha na Uislam zinampiga vita Mtume (s.a.w.w), lakini vilevile kuna pande hazina uhusiano na Uislam hazina uhusiano na Mtume (s.a.w.w) nazo vilevile zinampiga vita na zinamfanyia uadui Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni wajibu wetu sisi ni jukumu letu sisi kuweza kukabiliana na uadui huo na vita hizo ambazo zinazoelekezwa kwa Mtukufu wa daraja Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w). yamesemwa hayo juzi katika sherehe ya Maulid ya Mtume (s.a.w.w) iliyofanyika Masjid Al Ghadir Kigogo Post, Dar es Salaam.