Viongozi wakiwa meza kuu katika Sherehe ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) iyofanyika Kigogo Post, Dar es Salaam wa pili kutoka (kushoto) Sheikh Hemed Jalala kiongozi wa harakati ya Kiislam Tanzania.
Vijana wa Madrasa wakisoma Qaswida ya kumtukuza Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Madrasatul Sarafiyyah wakisoma Maulid ya Mtume (s.a.w.w) Kigogo Post, Dar es Salaam huku wakionyesha uhodari wao katika upigaji Dufu.
Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika hafla ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) iliyoandaliwa na uongozi wa Hawzat Al Imam Swaadiq (a.s) Kigogo Post, Dar es Salaam.
Waislam wametakiwa kuwa na moyo wa kuvumiliana baina yao kwani Mtume
(s.a.w.w) alikuja duniani kwa ajili ya kuwa rehema kwa viumbe vyote, pia
katika sherehe hiyo Sheikh Mkuu wa Tanzania Ithna Ashariyyah Sheikh
Abdallah Seif amewataka vijana kuto rudi nyuma katika kumsifu Mtume
(s.a.w.w) amesema maadui wa Maulid hawajui radha na faida ya kukumbuka
mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).