SEMINA JUU YA MADHARA YA MISIMAMO MIKALI YA IMANI ZA KIDINI (TAKFIRI).
Viongozi wa Kanisa la Garilaya liliyopo Msasani,Dar es Salaam akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hotel ya Lamada.
Katika Kongamano hilo ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lamada, Dar es Salaam, Viongozi wa dini wamewataka Waumini wa dini zote kujenga maadili ya kuvumilia baina yao kwani watakapokosa uvumilivu baina yao ndipo chanzo cha machafuko na kupelekea uvunjifu wa amani kila mmoja anawajibu wa kuhubiri dini kwa msingi wa mafundisho yake pia Waumini hao wametakiwa kuwafichua watu ambao wataonekana katika jamii kuwa ni wavunjifu wa amini kwani sio jukumu la jeshi la polisi peke yake kusimamia amani ya nchi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhary (Imam Bukhary Islamic Foundation) Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Waumini katika Semina iliyofanyia katika Hotel ya Lamada.
Waumini wa dini mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Lamada, Dar es Salaam wakisikiliza Semina juu ya "Madhara ya Misimamo mikali ya imani za Kidini (TAKFIRI) katika jamii na Taifa."
Katika upande wa nje wa Ukumbi kulioneka kukiwa na flemu zenye picha mbalimbali zinazoeneka na ujumbe mbalimbali juu ya matukio yaliyotokea duniani. Sikiliza hotuba iliyotolewa na Sheikh Hemed Jalala juu ya athari mbaya ya Uwahhab