Sheikh Waziri Nyello aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya Tanzania Shia Ithna Ashariyyah Community (T.I.C) ambayo Makao Makuu yake yapo Kigogo Post, Dar es Salaam, amesema kuwa lazima watu watambue Mawahhabi ni maadui wa Uislam na wao wamevaa joho la Uislam wanavaa Kanzu wanavaa Viremba na kuswali nakuendelea lakini wao wanamtumikia Marekani wengine kati yao wanajua kwamba ni vibaraka wa Marekani lakini wengi miongoni mwao bado hawajajua kwa hiyo itumike busara kuwaelimisha na kujadiliana nao ilituweze kuwatoa katika Uwahhabi kwa sababu wengi wao hawajui kama wanamtumikia Mmarekani wanaojua ni viongozi wao kwa hiyo tujitahidi kwenda nao taratibu mpaka tufikie lengo pia Sheikh Waziri Nyello amesema Mawahhabi ni mahodari wakuongea, mahodari wa vita wanajua kuteka Misikiti, kucheza Kareti wanajua kila kitu kwa sababu wanamkono ambao unawaangalia kwa hiyo ni jukumu letu kusimama imara huu ndio ulikuwa mchango wa Sheikh Waziri katika Kongamano la "Madhara ya Misimamo mikali ya imani za Kidini (TAKFIRI) katika jamii na Taifa." Kongamano ambalo liliandaliwa na Taasisi ya Imam Bukhary (Imam Bukhary Islamic Foundation) takribani siku mbili kuanzia J.mosi na J.pili lilijumuisha watu wa dini zote katika Hotel ya Lamada, Dar es Salaam.