Sayyid Aidarous Alawy: MAZAZI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).
Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliishi maisha yake yote na hamu yake yote kwa ajili ya Uislam kwa ajili yetu sisi kwa ajili ya binadamu wote kwa nini tusimsherehekee, kwa nini leo tusimkumbuke?
na ikiwa sisi twafurahikia kumsherehekea yeye kwanza tunarudisha wajibu tunarudisha shukurani tunasimamisha makumbusho ya mtu ambaye hafai kusauliwa katika dunia hii mtu ambaye kwamba akisaulika dakika moja maisha yetu yataenda kombo kwa sababu ukimsahau Mtume (s.a.w.w) umeisha usahau Uislam na ukiusahau Uislam unakuwa huna ubinadamu huna ulichobakia nacho sisi hatuna budi tumsherehekee kwa sababu yeye ni Rahma yeye ni Neema yeye ni fadhila na Mwenyezi Mungu (s) amesema: Tufurahikie fadhila za Mungu, tusherehekee Neema za Mungu, tuziinukie Neema za Mwenyezi Mungu.