Katika mapambano ya haki na batili, moja ya maadili muhimu ya mwanadamu ambayo kwayo Imam Hussein (a.s) alipata ushindi, ilikuwa ni "Ükombozi na Uhuru." Ama kwa Ukombozi, sifa hasa iliyo mbaya zaidi ni Utumwa. Yeye (a.s) alifanya juhudi dhidi ya utumwa na akaushinda kwa ushujaa, na hivyo kwa kunyanyua bendera ya uhuru na uwekaji huru watumwa, na kuiwasilisha kwenye ubinadamu. Mapmbano ya maadili ni ya kipekee katika muundo wake, silaha zake pia ni za kipekee na mtindo wa vita vilevile ni wa kipekee. Mtindo ambao kwamba Imam Hussein (a.s) alishinda vita hivi vya Ukombozi na kushinda maadili haya ya Ukombozi ni wa kipekee sana. Pamoja na moyo uliovutwa na umateka na damu iliyojaa uhanga, alipuliza roho katika maadili haya makubwa. Yeye (a.s) mwenyewe aliuawa shahidi, lakini aliwasilisha Ukombozi na uhuru kwenye Ummah. Alitoa Muhanga heshima ya Mwanawake, Watoto wa kiume na wa kike chini ya ufungwa wa mateka, ili Ummah upate wokovu kutokana na ufungwa wa dini na imani yao ya uwongo.
Wakati mwingine hushinda vita vya ufungwa katika njia ambayo kwamba ili kumfungulia mfungwa mmoja mpiganaji mwenyewe hufungwa kamba za ufungwa, ili kwamba aweze kuleta uhuru kwenye dini, ambayo iko chini ya ufungwa wa kutisha mno. Wakati mwingi shingo za wanadamu ziko huru, lakini akili, mawazo na imani zao ziko chini ya utumwa. Vilevile inawekana kwamba Ummah wote unaweza kuwa watumwa, na wakati Ummah wote unapokuwa watumwa, athari za utumwa huu vilevile zitadhihirika. Kama mtu akiwa mtumwa wa mtu, athari za utumwa huu kwa uwazi zitadhihirika zenyewe katika mtu huyu, kukomea kwake mwenyewe, lakini wakati Ummah wote na jamii wakiwa watumwa, athari ya utumwa huu itaonekana katika kiwango cha Ummah na Kijamii.
Imam Hussein (a.s) alishuhudia kwamba ni wakati ambapo watu binafsi na halikadhalika Ummah mzima na jamii ulikuwa umefungwa na utumwa na hivyo huamua kuifungua minyororo hii ya ufungwa. Kama inavyoonekana kwa wengine yeye (a.s) alilazimika kuweka minyororo, pingu na chuma kwenye shingo yake, kujifunga kamba katika mikono yake, lakini hata hivyo anafungua kamba na kuondoa kamba za utumwa daima ambazo zimeizunguka hadhi ya Ummah.
Kwa kuuawa shahidi yeye (a.s) mwenyewe ameihuisha heshima ya Ummah iliyokufa, na mpaka siku ya Hukumu ameonesha njia ya Ukombozi kwa Ubinadamu na Wokovu ulikuwa wa juu sana. Hivyo, kutokana na miongoni mwa majina yake mengi, vilevile hujulikana kama "Abu Ahrar", baba wa Ukombozi na hili limekuja katika Ziyarat kama: " Ewe kiongozi wa watu huru, Ewe baba na mlinzi wa wanadamu huru, salaam na amani iwe juu yako kutoka kwetu." Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi