"VIJANA WA ULAYA FANYENI UCHUNGUZI KUHUSU UISLAMU"

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa vijana wa Ulaya na Marekani akisema kuwa, matukio ya hivi karibuni nchini Ufaransa na matukio yanayoshabihiana na hilo katika baadhi ya nchi za Magharibi yamemlazimisha azungumze nao moja kwa moja.
Katika ujumbe wake huo sambamba na kuashiria njama zilizofanywa na Wamagharibi katika miongo miwili iliyopita kwa ajili ya kuidhihirisha dini ya Uislamu kuwa ni 'adui ana
yetisha', Ayatullah Ali Khamenei amesema inasikitisha kwamba, kuchochea hisia za hofu na chuki na kutumia mambo hayo, ni sera za muda mrefu katika historia ya siasa za Magharibi. Ameashiria historia ya hivi karibuni inayokemea mienendo isiyo ya kiadilifu ya serikali za Magharibi mkabala wa mataifa na tamaduni nyingine na kusema kuwa, historia ya Marekani na Ulaya kuanzia kipindi cha kuwafanya watu kuwa watumwa, kipindi cha ukoloni na dhulma dhidi ya watu wasio wazungu na wasio Wakristo, inaabisha.
Katika ujumbe huo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka vijana wa Ulaya na Marekani wawaulize wanafikra wao ni kwa nini dhamira ya umma inaamka kwa kuchelewa kwa miongo kadhaa au karne kadhaa? Na kwa nini jitihada zinafanywa ili kuzuia umma usielewe suala muhimu kama vile namna ya kuamiliana na fikra na utamaduni wa Kiislamu?
Ayatullah Khamenei amewataka vijana wa Ulaya na Marekani wafanye uchunguzi na uhakiki wa moja kwa moja na wao wenyewe kuhusu dini ya Uislamu ili kwa uchache watambue hicho wanachokikimbia na kukiogopa ni kitu gani? Chanzo cha habari:
http://kiswahili.irib.ir/…/46086-kiongozi-muadhamu-kwa-vija…