SABABU ZA UKANDAMIZAJI JUU YENU:

Busr ibn Abi Artaat alishambulia Yemen na Kabla ya hili alishambulia Madina pia. Alikaa juu ya Mimbari ya Mjumbe wa Allah (s.aw.w) na akawatusi Masahaba wake, akachoma nyumba, kisha alitoka Madina na akaendelea kushambulia sehemu nyingine. Katika hali hii alifika Yemen. Ubaidullah bin Abbas alikuwa Gavana wa Imam Ali (a.s) katika Yemen, kwa kiasi kwamba Busr ibn Abi Artaat aliwauwa watoto wawili wadogo wa Ubaidullah ibn Abbas mbele ya mama yao. Ubaidullah alikwenda Kufa pamoja na taarifa za kuuliwa watoto wake wawili ili haweze kumjulisha Imam Ali (a.s) kuhusu ukatili na mateso ya Busr. Moja ya mifano ya ukatili huu ilikuwa ni vifo vya watoto wake wawili ambao waliuliwa katika hali ya kutisha mno. Ubaidullah ibn Abbas alikuwa anatarajia kwamba Imam Ali (a.s) atamliwaza na kumpa mkono wa rambirambi kwa ajili ya watoto wake na kusoma Surah Fatiha.
Imam Ali (a.s) hakumchukulia mshambuliaji huyu muovu (Burs ibn Abi Artaat) kama mtu ambaye alikuwa anahusika na yote haya, baada yake aliwachukulia Masahaba wake kuwa chanzo cha kuingiwa na moyo kwa mvamizi kuja kutoka kote huko Damascus na kuvamia miji mpaka Yemen. Yeye Imam Ali (a.s) aliwakemea wote wawili Ubaidullah ibn Abbas na Said ibn Namran kwamba wao vilevile walikuwa na jeshi, basi kwa nini waliruhusu watoto wao wauawe? Kwa nini wasipigane na Busr? Imam Ali (a.s) alisema: "Kwa jina la Allah! Sasa nina hakika kwamba washambuliaji hawa waovu watachukuwa utawala kutoka kwenu, kama mtaendelea kuonesha uzembe wenu na udhaifu wenu kamwe hawataacha vitendo hivi vya ukandamizaji.
KUNA SABABU NNE ZA UKANDAMIZAJI DHIDI YENU:
1- Hamna umoja.
2- Hamumtii Imam wenu wa haki na mmemuasi Alla (s).
3- Hamuaminiki.
4- Mamuongezi idadi yenu na kukuza Umma wenu.

Wavamizi waovu nao pia wana sifa nne ambazo ziko kinyume kabisa na zile za kwenu:
1- Wameungana katika upotofu wao.
2- Ni waaminifu.
3- Ni watiifu kwa Kiongozi wao laghai.
4- Wanaongeza idadi ya watu na kukuza miji yao.

Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alionesha sababu za ndani nyuma ya ukatili huu, ingawa angeweza kwa urahisi kutaja sababu za nje, lakini alichosema yeye (a.s) kilikuwa ni: "Wavamizi jukumu lao ni kufanya mashambulizi na ukandamizaji, lakini ninyi mmewapa fursa washambuliaji hawa kutenda ukatili huu. Mmewaruhusu kuwakandamiza kwa sababu utengano wenu umekuwa msingi wa ruhusa hii. Wakati mnapokuwa sio waaminifu wa kutekeleza majukumu yenu, basi jihakikishieni kwamba mnatoa mwaliko kwa washambuliaji kutekeleza ukandamizaji. Kama hamuongezi idadi ya watu katika vituo vyenu, Misikiti yenu, Hussainiya zenu, na kama hizi zikiwa tupu basi vipengele hivi (vilivyotajwa) siku zote vitakuwa ni mwaliko kwa wavamizi hawa."
Mwenyezi Mungu anasema: "Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema yake mkawa ndugu, na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto naye akakuokoeni nalo. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyokubainishieni dalili zake ili mpate kuongoka." (Quran: 3:103)