UISLAMU UMEENEA KWA MAADILI YAKE MAZURI.

Kama tutafikiri habari hii kwama Bibi Khadija (a.s), ambaye hapana shaka alikuwa tajiri mkubwa, na utajiri wake wote na rasilimali yake yote ilitumika kwa ajili ya Allah na kwa faida ya Uislamu tu. Lazima pia tutafakari juu ya ukweli kwamba Bibi Khadija (a.s) alikuwa tajiri wa Makka na sio yule wa Karachi. Kuna tofauti kubwa kati ya Bibi tajiri wa Makka wa wakati ule na Bibi wa Karachi leo. Mawazo yetu mtu fulani kuwa tajiri leo ni tofauti sana na ufafanuzi wa mtu kuwa tajiri katika siku hizo. Kwa mtazamo wa kijamii, Makka ulikuwa ni mji mdogo na ulikuwa ni sawa na kijiji cha wakati wetu huu. Yalikuwepo makundi fulani  miongoni mwa washirikina, moja wapo lile la wafanya biashara, hivyo kulikuwa na idadi ndogo ya wafanya biashara na hao walikuwa watu ambao walikuwa hawafanyi kazi kwa mtu yeyote kama vibarua. Watu hawa ambao walikuwa hawakuajiriwa na mtu yeyote na walikuwa na biashara zao binafsi walichukuliwa kama matajiri.

Hivyo, Bibi Khadija (a.s) vilevile alikuwa Bibi tajiri wa Makka kwa misingi hiyo hiyo, lakini dhana ya kuwa tajiri na utajiri ambayo tunayo leo kwa lugha ya Mamilioni na Mabilioni sio kweli kwa zama hizo. Kwa hiyo sio katika hali tunayofikiria na kuwaza, kwamba alikuwa Milionea na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w) amemuoa kwa ajili ya utajiri wake. Falsafa ya ndoa hii ilikuwa juu ya misingi ya maadili waliyokuwa nayo watu hawa wawili. Bibi Khadija (a.s) alishuhudia Uaminifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na yeye (s.a.w.w) alishuhudia usafi na adabu yake, na hivyo ilikuwa ni ndoa kati ya Uaminifu na Usafi na sio ndoa kati ya uroho na utajiri. Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi