Zikiwa zimekaribia
siku za Mwenyezi Mungu za Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa
Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yanayoanza siku aliporejea kishujaa
nchini Iran, Imam Khomeini (MA), Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei,
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi amekwenda
kufanya ziara katika Haram ya mwanachuoni huyo mkubwa, na sambamba na
kumsomea al Faatiha, amemuenzi na kumuombea dua mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Vilevile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefanya ziara
kwenye makaburi ya mashahidi wa Tir 7 -kwa mwaka wa Kiirani wa Hijria
Shamsia- na kwenye makaburi ya mashahidi wengine ya Behesht Zahra
-kusini mwa Tehran-, na kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu awapandishe
daraja za juu mbele Yake.
Itakumbukwa kuwa siku ya Al khamisi ya Februari 1, 1979, Imam Khomeini (MA) alirejea nchini Iran kutoka uamishoni nchini Ufaransa, na kurejea kwake huko kulitia nguvu harakati za mapinduzi ya wananchi wa Iran yaliyoung'oa madaraka utawala wa kidikteta wa Shah, Februari 11, 1979. Siku hizo kumi za baina ya kurejea nchini Iran Imam Khomeini (MA) hadi kupatikana ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu ni maarufu kwa jina la Dahe Fajr yaani Alfajiri Kumi na huadhimishwa kila mwaka. Sherehe hizo hufikia kileleni Februari 11, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Bahman 22. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/46245-kiongozi-azuru-haram-ya-im…