Leo kama Shia anauawa popote ni kwa ajili ya jinai kwamba yeye ni Shia,
kwa jinai ambayo wanachukua jina la Hussein (a.s). Hii ndio jinai ambayo
kwamba inawafanya wauawe. Watu wanasema tunapigwa, kuuliwa na kutiwa
nguvuni na vyombo vya dola ni kwa sababu ya kuunga kwetu mkono
Mapinduzi ya Kiislam ya Iran. Hii ni adhabu yetu kwa ajili ya kuunga
mkono na kuthibitisha Mapinduzi ya Kiislam. Wanasema kwamba sasa lazima
tuache na tusimamishe uungaji huu mkono ili tuweze kuwa salama.
Wamesema sawa lakini wamelishikilia tatizo hili sehemu yake ya mwisho
kabisa, kwa nini hawaendi mbali kidogo kwenye kiini cha tatizo.
Watatambua kwamba hawapigwi kwa sababu ya kuunga kwao mkono Mapindizi ya
Kiislam, mnauawa kwa sababu ya kuchukua jina la Hussein ibn Ali (a.s).
Kama mnadhani kwamba kuacha mapenzi na kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislam
ni ufumbuzi kwa ukombozi wenu basi ni bora kumwacha Hussein ibn Ali
(a.s) na mtakuwa salama kabisa na hakuna atakayekuwa na wasiwasi na
ninyi. Kwa nini muishilizie matatizo ya jamii na Mapinduzi ya Kiislam ya
hivi karibuni, nendeni kwenye sababu ya Mapinduzi ya Kiislam ambayo
yalikuwa ni njia ya Imam Hussein (a.s), na hata nendeni zaidi kwenye
chanzo ambacho kilikuwa ni Uislam. Ni bora mtangaze kwamba amna habari
na Uislam na mhakikishe kwamba hakuna mtu atakaye wasumbua na
kuwasababishia matatizo. Leo misiba iko juu ya Waislam ulimwenguni pote,
ni kwa sababu ya dini yetu, Hivyo achaneni na Uislam wenyewe na mtakuwa
salama kutokana na matatizo yote.