Leo katika Pakistan kuna Mamilioni ya Mashia ambao wamejitengea majukumu
yao kwenye kubeba Maiti na kuzizika tu. Kazi yao ni kusoma Surah Fatiha
kwa ajili ya Mashahidi. Kwa nini magaidi wachache wamezingira Mamilioni
yao? Sababu yenyewe ni kwamba Mamilioni haya yapo lakini ndani ya
nyumba zao, madukani mwao, maofisini; hawapo pale ambapo wanatakiwa
kuwepo. Hata kama wangekuwepo vijana mia moja tu nje katika uwanja basi
hakuna atakaye thubutu kugusa jumuiya hii. Jumuiya inakuwa
mwathirika na misiba na hatari wakati hakuna mtu wa jumuiya hiyo
aliyepo katika uwanja. Si wanachuoni wao wala wasio wanachuoni, wala
wanaume au wanawake wao hakuna aliyepo katika uwanja.
Karbala ni uwanja wa uwepo na tayari. Kiongozi wa Mashahidi (a.s) alichukua wanawake kwenda Karbala kuonesha kwamba jukumu la mwanamke sio kukaa tu ndani ya kuta nne za nyumba, bali badala yake lazima awepo katika kila uwanja ambako wanawake wanaweza kuwepo. Imam Hussein (a.s) hakushawishiwa na mtu yeyote kuwachukua wanawake na kuwa pamoja naye, angeweza kuwaacha, lakini kama asingewachukuwa Karbala isingekamilika, madhumuni ya Karbala yasingekamilishwa. Wanaume wangeuawa lakini ujumbe wa Karbala usingeufikia ulimwengu. Hii ndio sababu Kiongozi wa Mashahidi (a.s) alitengeneza vikosi viwili, kimoja kikosi cha Hussein (a.s) na kingine kikosi cha Zainab (a.s). Jukumu la kikosi cha Hussein (a.s) liliisha katika mkesha wa Ashura wakati ambapo jukumu la kikosi cha Zainab (a.s) lilianza kuanzia mkesha wa Ashura na kuendelea mpaka Kiyama. Hivyo wote wanahitajika katika uwanja huu; bila ya wanawake hawapo uwanjani, jumuiya hii ya Mamilioni itaendelea kubeba maiti. Nasaba hii ya kubeba maiti itaisha tu siku ile wakati vijana wa jumuiya hii watakapokuwa wamejiandaa na kuingia uwanjani, na kwa kushuhudia utayari wao maadui watakimbilia ndani ya nyumba zao. Leo ni kinyume cha mambo ambapo tumekaa ndani ya nyumba zetu na maadui wako nje uwanjani. Lakini Allah ameahidi kwamba kama waumini wakikaa ndani ya nyumba zao basi Allah ataleta Umma ambao utatembea kwa miguu yao wenyewe kuelekea kwenye uwanja wa mapambano; watapigana vita katika njia ya Allah, hawataogopa kifo na lawama. Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi