Shambulizi la kigaidi la hapo jana lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Taliban dhidi ya shule moja inayomilikiwa na jeshi la Pakistan limeendelea kulaaniwa na viongozi mbalimbali kote duniani. Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya ndani na nje ya Pakistan pia yamelaani shambulizi hilo lililopelekea kuuawa watu 141 wengi wao wakiwa wanafunzi. Magaidi wa kundi linalojiita Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP) walivamia shule hiyo katika mji wa Peshawar na kuwamiminia risasi wanafunzi pamoja na walimu. Baada ya makabiliano ya silaha magaidi hao waliuawa lakini tayari walikuwa wamesababisha maafa makubwa.
Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif, mbali na kulaani vikali shambulizi hilo, amesema serikali yake itakutana na viongozi wote wa kisiasa, kidini pamoja na wale wa kikabila ili kujadili hatua za kuchukuliwa dhidi ya magaidi hao wa TTP. Nawaz Sharif amesema mkutano huo unaofanyika leo Jumatano utajadili pia hatua za muda mrefu zitakazochukuliwa na serikali kwa ushirikiano wa makundi yote ya Pakistan ili kuzuia kujikariri shambulizi kama hilo katika siku za usoni. Kiongozi huyo ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia shambulizi hilo.
Shambulizi la hapo jana dhidi ya wanafunzi na walimu wasio na hatia huko Peshawar limevunja ukuta wa kisiasa uliokuwa umewagawa wanasiasa wa serikali na upinzani kwani tayari kiongozi wa chama cha upinzani cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, Imran Khan ametangaza kusitisha maandamano ya wafuasi wake dhidi ya serikali na kutoa wito kwa taifa kuungana na kuwa kitu kimoja wakati huu wa msiba. Imran Khan ambaye kwa muda sasa amekuwa akiongoza maandamano ya umma dhidi ya serikali ya Nawaz Sharif amekubali kuhudhuria mkutano wa leo mjini Islamabad. Kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa amesema vyombo vya usalama, serikali na Wapakistani wote wanapaswa kuchukua msimamo wa pamoja wa kukataa vitendo vya kigaidi na vya kinyama vinavyofanywa na magaidi wa TTP.
Mauaji ya hapo jana dhidi ya makumi ya wanafunzi na walimu katika shule inayoendeshwa na jeshi huko Peshawar pia yamelaaniwa na viongozi wa eneo na wale wa kimataifa. Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema unyama uliofanywa na kundi la Taliban la Pakistan haukubaliki na ametaka watenda jinai hiyo wafuatiliwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Naye Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini amesema dunia inapaswa kupinga ugaidi kwa kinywa kipana na sio tu kwa maneno bali pia kwa vitendo. Viongozi wa nchi zingine kama vile Afghanistan, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, India na kadhalika wametoa rambirambi zao kwa serikali na watu wa Pakistan kufuatia hujuma hiyo ya magaidi. Taarifa ya Rais wa Iran, Hassan Rouhani, imesema ugaidi na misimamo mikali ni tatizo la kimataifa linalopaswa kupigwa vita na nchi zote duniani. Taarifa hiyo imsesisitiza udharura wa kutangazwa vita vya dhati dhidi ya ugaidi duniani pasina kuweko malengo ya kisiasa ya watu binafsi au nchi fulani.
RAIS WA IRAN: NI WAZI SYRIA INAPAMBANA NA MAGAIDI.
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kuwa, dunia sasa imetambua kuwa serikali na wananchi wa Syria wanapambana na makundi ya kigaidi na dhidi ya njama za kigeni. Rais wa Iran amesema hayo alipokutana na kuzungumza na Wael Nadir al Halqi Waziri Mkuu wa Syria hapa mjini Tehran. Dakta Rouhani ameongeza kuwa, jinai zinazotekelezwa na makundi ya kigaidi nchini Iraq zimeweka wazi utambulisho wa magaidi na njama zilizoratibiwa na adui dhidi ya dini ya Uislamu na eneo la Mashariki ya Kati. Rouhani amesisitiza kwamba, mgogoro wa Syria unaweza kutatuliwa tu kwa mazungumzo ya kisiasa ya pande za ndani ya nchi hiyo.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Syria ameishukuru Iran kwa kuiunga mkono nchi yake na kusema kwamba Damascus iko tayari kupokea njia yoyote inayofaa ili kutatua mgogoro unaoendelea nchini humo, njia ambayo itaimarisha umoja na kutokiuka haki ya kujitawala ya Syria.
JESHI LA ISRAEL LASHAMBULIA WAOMBOLEZAJI PALESTINA.
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia raia wa Palestina waliokuwa katika shughuli za mazishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwajeruhi watu 30. Ghasia ziliibuka karibu na kituo cha upekuzi cha Qalandiya ambako wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi za plastiki waombolezaji wa Kipalestina baada ya marasimu hayo ya mazishi kugeuka hapo jana na kuwa maandamano ya kupinga ukaliaji mabavu wa Israel.
Wapalestina waliojeruhiwa walifikishwa hopistalini huko Ramallah na wengine walipatiwa matibabu kaika eneo palipozuka ghasia. Wapalestina zaidi ya 10,000 jana walishiriki katika mazishi ya Mahmoud Adwan kijana wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 21, ambaye aliuliwa katika shambulio la wanajeshi wa Israel katika kambi ya wakimbizi ya Qalandiya mapema hapo jana.