Kundi la
wanamgambo wa kitakfiri na kigaidi la Daesh limewaua zaidi ya madaktari
50 katika mji wa Mosul, nchini Iraq. Mohammad Chalabi mmoja kati ya
viongozi wa eneo la Mosul amesema kuwa, hivi karibuni kundi la kitakfiri
na kigaidi la Daesh lilianzisha operesheni kamambe kwa minajili ya
kuwakamata madaktari na madaktari bingwa katika mji huo na hatimaye
kuwaua zaidi ya madaktari 50 katika mji huo. Chalabi ameongeza kuwa, magaidi hao walitekeleza unyama huo wa kutisha wa kuwauwa madaktari hao, baada ya kuwafyatulia risasi vichwani.
Wakati huohuo, jeshi la Iraq limefanikiwa kuwaangamiza makumi ya
magaidi katika operesheni kamambe iliyofanyika katika mkoa wa
Salahuddin. Taarifa za jeshi zinaeleza kuwa, wanajeshi wa serikali
wakishirikiana na wanamgambo wa kujitolea wamefanikiwa kulikomboa eneo
la Sayyid Gharib lililoko kati ya miji ya Balad na Dajil kusini mwa mkoa
wa Salahuddin. Jeshi la Iraq limeeleza kuwa, kukombolewa kwa eneo hilo,
kutapelekea kukombolewa kikamilifu maeneo ya kusini mwa mji wa Takrit,
unaodhibitiwa na makundi ya kigaidi. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/44844-daesh-waua-zaidi-ya-madakt…
MKUU WA AL-AZHAR ALAANI JINAI ZA MATAKFIRI.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar mjini Cairo Misri amelaani vikali jinai zinazofanywa na makundi ya kitakfiri duniani hasa kundi la Daesh (ISIL).
Akizungumza leo katika ufunguzi wa 'Kongamano la Kimataifa la Kupambana na Misimamo Mikali ya Kidini' katika mji mkuu wa Misri, Sheikh Ahmed al Tayeb amelaani vikali 'jinai za kinyama' zinazofanywa na kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria. Mwanazuoni huyo wa ngazi za juu wa Kisuni amesema magaidi wa Kitakfiri wanaeneza taswira potofu kuhusu Uislamu duniani. Ameongeza kuwa "wakitumia bendera ya dini tukufu ya Kiislamu, wamejippaciha jina la 'Dola la Kiislamu' katika njama zao za kueneza Uislamu bandia." Sheikh Al Tayeb amezungumzia pia sababu za kidini, kisiasa na kiuchumi za kuibuka makundi ya kigaidi katika nchi za Kiislamu. Amesema wanazuoni wa Kiislamu nao pia wanabeba lawama kutokana na kutotekeleza majukumu yao na hivyo kupelekea kuibuka misimamo mikali ya kidini na makundi ya kigaidi kama al-Qaeda. Akiashiria madai ya Marekani kuwa imeunda muungano wa kukabiliana na makundi ya Kitakfiri Iraq na Syria, Sheikh Al Tayeb amesema, Marekani inapaswa kukabiliana na nchi ambazo zinaunga mkono magaidi kifedha na kijeshi.

Wanazuoni kutoka nchi kadhaa zikiwemo Iran, Saudi Arabia na Morocco
wanashiriki katika mkutano huo ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Al Azhar.
Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/44914-mkuu-wa-al-azhar-alaani-ji…