Zaidi ya
mashirika 35 ya kutetea haki za binadamu yameitaka serikali ya Bahrain
kumwachia huru Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha al-Wifaq, Sheikh
Ali Salman aliyekamatwa jana Jumapili.
Taarifa ya pamoja ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kutoka nchi za Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani imesema kuwa, hatua ya kukamatwa Sheikh Salman inakiuka haki yake ya kujieleza. Taarifa hiyo imeuonya utawala wa familia ya Aal Khalifa ikisema hatua yake hiyo inaweza kuitumbukiza Bahrain katika lindi la machafuko mapya.

Kiongozi huyo wa upinzani aliwekwa kizuizini hapo jana baada ya
kuhojiwa mchana kutwa. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain imesema
kwamba, Sheikh Ali Salman anazuiliwa kwa kukiuka sheria za usalama.
Viongozi wa kidini, wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na mashirika ya kiraia nchini Bahrain yametishia kufanya maandamano makubwa ya kitaifa iwapo utawala wa kifalme wa Bahrain hautamwachilia huru Katibu Mkuu wa al-Wifaq. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/45524-bahrain-yatakiwa-kumwachia…
POLISI YA BAHRAIN YAMKAMATA KATIBU MKUU WA AL WIFAQ.
Ghasia na machafuko yametokea Manama mji mkuu wa Bahrain baada ya askari usalama wa utawala wa Aal Khalifa wa nchi hiyo kumkamata Sheikh Ali Salman Katibu Mkuu wa Jumuiya ya al Wifaq nchini Bahrain. Taarifa zinasema kuwa, Sheikh Ali Salman amekamatwa na polisi wa utawala wa kifalme kwa kwa madai ya kufanya uchochezi na kuzusha ghasia na machafuko dhidi ya serikali pamoja na kupanga njama za kuuangusha utawala huo wa kifalme. Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya al Wifaq ya Bahrain imeeleza kuwa, kitendo cha serikali ya Bahrain cha kumtia mbaroni Sheikh Salman ni cha hatari na hakikubaliki kisheria.Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wananchi wa Bahrain wataendelea kufanya maandamano ya amani hadi yatakapotekelezwa kikamilifu matakwa yao. Sheikh Ali Salman ametiwa mbaroni ikiwa imepita siku moja tu tokea ulipoitishwa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo na kumchagua tena kuwa Katibu Mkuu wa al Wifaq kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu ya ndani na nje ya nchi yamelaani kitendo cha serikali ya Bahrain cha kumtia mbaroni Sheikh Ali Salman. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tokea mwaka 2011 wananchi wa Bahrain wanaendesha maandamano ya amani dhidi ya utawala wa kifalme wa Aal Khalifa wakishinikiza yafanyike mabadiliko ya kisiasa nchini humo.