Assalaam Aleykum, Unaarifiwa hitima ya Sheikh Abdul Qadir Sudi Muwaya
(Doktoor Abdul Qadir) aliyefariki Uganda kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana alipokuwa akitokea Msikitini, kisomo kitafanyika siku ya
Alhamisi ya tarehe 1/01/2015 Saa 4 Asubuh katika Msikiti wa Khoja Shia
Ithna Ashariyyah uliyopo mjini Posta kwa watakao penda kushiriki katika
dua ya kumuombea ndugu yetu usafiri utakuwa Masjid Al Ghadir Kigogo Post
kwa Sheikh Hemed Jalala kuanzia Saa 3 Asubuhi.
Sheikh Abdul Qadir alikuwa kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu ya Ahlul Bait (ABIF) marhumu Sheikh Abdul Qadir ambaye alifahamika zaidi kwa jina la Doktoor Abdul Qadir alisimamia ujenzi wa misikiti 50 katika maeneo mbalimbali nchini Uganda na kudhamini gharama za masomo kwa watoto wasio na uwezo. Marhumu Abdul Qadir alizikwa siku ya Ijumaa katika Wilaya ya Mayuge mashariki mwa Uganda. "Hakika sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea."