WAISLAM WA MADHEHEBU YA SHIA ITHNA ASHARIYYAH NCHINI NIGERIA WAMEUNGANA NA WAISLAM WENZAO ULIMWENGUNI KOTE KATIKA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MJUKUU WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W) IMAM HUSSEIN (A.S)

 Imam Abu Shuhadaa Hussein bin Ali (a.s) aliitoa muhanga nafsi yake, ahali zake, mali zake na vengine vinavyohusiana naye kwa ajili ya Uislamu, hivyo kuna umuhimu kwa Waislamu kujua mwamko huu Mtukufu kwanza, pili wamuunge mkono kwa aina zote za msaada na tatu wachukue kigezo kwa Imam wao katika kujitoa muhanga kwa ajili ya Uislamu. Na Muislamu ajue kwamba kujitoa muhanga ni katika vitu vinne, na Imam alijitoa muhanga kwa mambo haya manne katika mapambano ya KARBALA:- 

 1- Kujitoa muhanga katika nafsi. 
 2- Kujitoa muhanga katika ahali. 
 3- kujitoa muhanga katika mali. 
 4- Kujitoa muhanga katika umaarufu wake.

 Imam alijitoa muhanga katika nafsi yake akauliwa. Alijitoa muhanga katika ahali zake mpaka likauliwa kundi miongoni mwao, na wengine wakatekwa. Alijitoa muhanga katika mali zake ambapo aliporwa. Alijitoa muhanga katika umaarufu wake mpaka wakamwita Khawariji na wakamlaani juu ya mimbari. Ni kweli ilikuwa hivyo kwa muda mchache kama ambavyo ni kawaida katika udanganyifu na tuhuma, hivyo ni lazima kwa mwanajihadi asiogope kuvunjika kwa umaarufu wake kama atapigana kwa ajili ya kutengeneza. Kwani Mwenyezi Mungu ndio mwenye kuafiki na kutakwa msaada. Na Muhammad Al - Husayn As - Shirazi