Waumini
wa dini ya Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah leo wameazimisha
Kitaifa Kifo cha Mjukuu wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa
matembezi ya amani yaliyofanyika Kigogo Post, Dar es Salaam. Imam
Hussein (a.s) aliuawa katika jangwa la Karbala huko Iraq mnamo mwaka wa
61 Hijjiria kwa ajili ya kupigania haki na utu wa mwanadamu.