Mubalighina
hawana budi kufuata nyayo za Sheikh Twahiru Abdallah Imam wa Masjid Al
Kisaa na mwalimu wa Madrasa katika Mkoa wa Tanga Wilaya ya Lushoto yeye
mbali na kufanya kazi ya kueneza mafundisho sahihi ya dini ya Kiislam
katika Wilaya ya Lushoto anajishughulisha na masuala ya kilimo ili
kukizi mahitaji yake binafsi na familia yake leo hii imekuwa ni hajabu
kuona baadhi ya watu wanafanya kazi ya
dini ni sehemu ya kujipatia kipato ili kukizi mahitaji binafsi hii ni
njia mbaya Mubalighina anatakiwa kujishughulisha sio katika kazi ya dini
tu bali hata kazi binafsi ili haweze kuendesha maisha na harakati kwa
ujumla bila ya hivyo kazi ya kuendesha harakati ya dini kila siku
itabaki kuwa ni kiini macho bila ya mafanikio jamii inahitaji kuona
mfano kutoka kwa watu wa dini hasa katika masuala ya maendeleo Mubalighi
wanatakiwa kujitambua kuwa Mubalighi sio maana kukaa bila ya kuwa na
shughuli maalumu tunaona hata Maimam wenyewe walikuwa na shughuli za
kufanya mbali na kazi ya kuendesha harakati za kidini. Ibnu Abbas
anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa amuonapo mtu na akavutiwa naye,
husema: "Je ana kazi?" Wakasema hana, husema: " Hana thamani tena
machoni kwangu." Wakamuuliza kwa nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?
Akasema: "Kwa sababu Muumini asipokuwa na kazi ataishi kupitia dini
yake." Rejea: Jamiul - Akhbar: 390/1084.