Kuna sababu
nyingi sana nyuma ya hili. Watu wengine ni kutokana na ujinga, wengine
kwa shaka za kuundwa, wengine kutokana na sababu nyinginezo na wengine
wamepotoshwa na maadui. Kwa maneno mengine, baadhi ya watu wanaposhwa na
mawakala wasaliti ambao wamepandikizwa miongoni mwetu ili kuiziba njia
hii. Mawakala hawa wanapandikizwa kutokea nyuma na wanapelekwa kwenye
mimbari zetu ili kubadili mwelekeo wa jumuiya hii, lengo
kuu ni kuukengeusha Umma huu kutoka kwenye mfumo wa maisha wa Kimungu.
Ninawasilisha hapa kisa cha kweli kama mfano kwa ajili yako ili upate
kuelewa yale yote yaliyofanywa ili kuwapotosha watu kutoka kwenye
Wilayatul - Faqiih. Ungeziona na habari pia jana kwamba, ili kubadilisha
mfumo wa utawala nchini Syria, Serikali ya Marekani imetenga bajeti ya
dola Milioni tano za Kimarekani. Na ili kubadili Serikali nchini Iran
Marekani imetenga dola za Kimarekani Milioni ishirini na moja kwa kila
mwaka. Pesa hizi wanampa nani? Wanazitoa kwa mawakala kama hawa ambao
watakuja kuzungumza dhidi ya mfumo huu wa Wilayat, kuandika chochote na
kuendelea kufanya chochote dhidi ya mfumo wa Wilaya. Waliunda baraza
huko Marekani kwa jina la UMAA chini ya mwongozo wa Paul Wolfowitz. Huyu
Paul Wolfowitz alikuwa ndiye mtaalamu wa ushauri wa mashambulizi ya
Marekani huko Iraq. Yeye alibuni shambulizi hili na kisha akalipanga
yeye. Chini ya uongozi wake waliunda kamati yenye Ulamaa, Makhatibu wa
Kidini na wenye kushikilia mimbari. Lengo la baraza hili ni kufanya kazi
kuelekea kwenye kuyasafisha mawazo ya Imam Khomein (R.A) kutoka kwenye
Madhehebu ya Shi'ah. Wao walisema kwamba mambo fulani ndani ya Madhehebu
ya Shi'ah yameingia kutoka nje na haya ni lazima yaondolewe. Paul
Wolfowitz wakati akiwa Mkuu wa Benk ya Dunia alijitokeza kwenye Tv akiwa
na sura zinazojulikana sana za watu wa jumuiya ya Shi'ah wakiwa wamekaa
pamoja naye. Alisema kwamba mawazo ya Imam Khomein (R.A) yanapaswa
kuondolewa kutoka kwenye jumuiya ya Shi'ah. Wametenga Mamilioni ya dola
kwa ajili ya shughuli hii. Kwa hiyo sio kwamba kama mtu akikaa kwenye
mimbari na kuzungumza dhidi ya Wilaya, basi huo ni uharibifu wa mawazo
na akili yake mwenyewe, laahasha. Ukifuatilia mahusiano ya mtu kama huyo
yatarudi nyuma mbali kabisa, baadhi ya ofisi za Kibalozi, au NGO fulani
zitakuwa nyuma yake huyo. Hivyo inatubidi tuwe na tahadhari na uwerevu.
Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi