Waumini
wa dini ya Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah leo wameungana na
Waislam wenzao ulimwenguni kote kusherehekea Ushindi wa tukio la
Mubahala, Sherehe hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Marehemu Sheikh
Dhikir Kihondo Temeke jijini Dar es Salaam kukifuatiwa na dua maalumu ya
kumrehemu Sheikh Dhikir Kihondo ambaye ni Muasisi wa taasisi ya
Tanzania Ithna Ashariyyah Community (T.I.C) ambayo hivi sasa Makao makuu
yake yapo Kigogo Post jijini Dar es Salaam .
Sheikh Hemed Jalala amesema katika sherehe hiyo : kitendo cha Mtume (s.a.w.w) kutoka na watu wanne na asiwachague watu wengine wakawaida akakae meza moja na Manaswara baada ya kushindwa Manaswara na Mtume (s.a.w.w) akaacha kuwatoa manaswara katika ardhi ya Madina wakabakia kuishi katika mji wa Najiran siku ya Mubahala ni siku ya kujifunza hekima, hekima hii ni moja ya mambo aliyoyafanya Marehemu Sheikhe Dhikir Kihondo alipowaona watu waliotawanyika hawana mwamvuli hawana kitu cha kuwakusanya akawatengenezea Taasisi ya Tanzania Ithna Ashariyyah Community (T.I.C) ili haweze kuwakusanya ni hekima kubwa na busara kubwa katika siku ya Mubahala hekima hii inaitaji kuenziwa na kutunzwa hekima na mbinu na falsafa za kuwakusanya watu Mtume (s.a.w.w) angeweza kutoka kufanya mdahalo peke yake lakini Mtume (s.a.w.w) aliwakusanya watu akatoka na watu yeye akiongoza msafara, Waislam watashinda Waislamu wataonekana watendaji wazuri watakapokuwa wamekusanywa na mwamvuli wao mmoja Waislam watakuwa tishio duniani na wataheshimiwa ndani ya nchi zao watakapoitumia falsafa na hekima ya Mtume (s.a.w.w) ya kukaa na watu ambao wanatofautiana nao kiitikadi wakakaa nao meza moja wakazungumza nao Mtume (s.a.w.w) alikuwa na uwezo wa kuwafukuza Wakristo wa Najiran lakini Mtume (s.a.w.w) alikaa nao meza moja akakaa nao Madina Mtume (s.a.w.w.)hajawalazimisha Wakristo wa Najiran waingie katika Uislam ambapo alikuwa na uwezo wa kunyanyua upanga na kuwaambia tamkeni shahada mbili akuwalazimisha kwa sababu hakuna kulazimishana katika dini ni makosa makubwa kuwepo fikra kwamba ni lazima kuwasilimisha watu kwa nguvu wawe Waislam ni makosa makubwa hakuna katika Uislam, Uislam hausemi ya kwamba twende tukawauwe watu hili wawe Waislam vita vyote alivyopigana Mtume (s.a.w.w) vilikuwa ni vita vya kujilinda Warabu walimkataza Mtume (s.a.w.w) asitangaze neno la Mungu kwa makatazo hayo alipambana nao Mtume (s.a.w.w) hajatoka kuwapiga watu waingine, Wakristo wa Najiran waliposhindwa Mtume (s.a.w.w) hajawaambia kwamba ingieni katika Uislam kwamba lazima muwe Waislam au nitawauwa bali Mtume (s.a.w.w) aliwaambia mkiingia katika Uislam mna haki zote kama Waislam wengine wakawaida katika kumbukumbu ya kuukumbuka ushindi wa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul Bayt (a.s) kwa manaswara wa Najiran tujifunze hekima hii kubwa ya kuvumilia kuweza kukaa pamoja na adui bali na mtu ambaye unatofautiana naye kukaa katika meza moja falsafa hii na hekima hii itafanya watu tuwabadilishe tuwalete katika mlengo wa Mtume (s.a.w.w) ukiisoma harakati ya Mtume (s.a.w.w) ya kukaa na Wakristo wa Najiran meza moja inakusomesha kitu muhimu inakusomesha ya kwamba mkitaka harakati yeyote ifeli iwe ni harakati inayotumia hisia.
Harakati yeyote itakapokuwa inapelekwa kwa hisa kwa matukio yanayotokea au kuna jambo limetokea tunaathirika tayari tunataka kuingia barabarani tayari kwa kuandamana harakati hiyo haifanani na harakati ya Mtume (s.a.w.w) na harakati ya Ahlul Bayt (a.s) hekima busara na akili kutambua mazingira ndio tunachokisoma katika tukio la Mubahala.