Asalaam Aleykum, Enyi Waislam na Wapenda haki ulimwenguni mbona mmekaa
kimya katika ardhi ya Tanzania kama kwamba hakuna jambo lolote
linalotendeka ulimwengu utawala wa Saudia umetoa adhabu ya kifo kwa
Sheikh Nimr je, adhabu hii ya kifo kwa Sheikh Nimr Baqer Al Nimr ni haki
yake? Na kama sio haki yake sisi kama Waislam na wapenda haki
ulimwenguni tunasema nini juu ya utawala huu unaokiuka haki za binadamu?
Ndugu zangu tuangalie asije Sheikh Nimr akatulingania kama Bibi Zainab
(a.s) akasema: " Enyi viumbe wakimya! Hamna haki ya kulia juu yangu.
Ninyi ni miongoni mwa maadui zangu. Niliuawa kwa ajili ya ukimya wenu.
Shahidi mshuhuda wa ukandamizaji unaofanywa na wakandamizaji; ni
mshuhuda wa mauaji ya wauaji na mshuhuda wa ukimya wa watazamaji.
Shahidi atayasema haya mbele ya Allah kwamba: "Ewe Mola wangu! Wakati
nilipokatwa kichwa na mwili wangu kukatwakatwa vipande, ni kwa maelezo
ya nani lilifanywa hili na ni nani waliokuwa wamekaa na kuangalia hili
kama watazamaji?" Ni jukumu la kila mmoja wetu kulaani kitendo
kinachofanywa na utawala wa Aal Saud juu ya ukiukwaji wa haki za
binadamu. "Kukaa kimya ni sawa na kuunga mkono dhulma" Imam Khomeini
(R.A)