"Wala usidhani wale walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu, bali ni hai wanaruzukiwa kwa Mola wao." (Al Imran Aya 169). Mwezi wa Muharram upo njiani tuutumie mwezi huu kukuza imani zetu. Karbala inatufunza maisha namna ya kuishi sio kuomboleza na kula Nihazi tu ni jukumu letu kuchukua mafunzo ya Karbala na Siku ya Ashura ili tuweze kuishi maisha bora kama jamii iliyohai na sio jamii ya kitumwa Imam (a.s) alitoka yeye na kizazi chake na jamaa zake kwa ajili ya kuchukia udhalili na ukandamizaji dhidi yetu na sisi hatuna budi kuenzi na kufuata nyayo za watu hawa. Karbala ni uwanja wa maisha na hii maana yake ni kifo cha Kishahidi. Kifo cha Kishahidi maana yake ni maisha halisi ya mwanadamu, sio maisha ya kula nafaka na chakula. Shahidi ameacha vitu vyote hivi lakini bado Allah anasema anapata riziki. Riziki hii sio chakula kwa ajili ya tumbo lakini riziki ya maadili, sifa njema na heshima. Shahidi ni yule mtu mwenye kujiheshimu ambaye hufundisha watu njia ya kuishi maisha. Mshipa wake wa Shingo hukatwa kwa sababu hataki kuishi kama mnyoo ndani ya mzoga. Shahidi huzihuisha jumuiya na jumuiya hupata somo la maisha kutoka kwa Mshahidi. Lakini kama watu wakiogopa baada ya kusikiliza habari za kifo cha Kishahidi, kwa watu kama hao Allama Iqbal anasema: "Mtu ambaye moyo wake hutetemeka juu ya habari za kifo cha kafiri ambaye anaweza kumwambia afe kifo cha Mwislamu, watu kama hao kamwe hawawezi kufa kifo cha kweli cha mwanadamu na Mwislamu." Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi