TAASISI YA BILAL MUSLIM MISSION IMEFANYA SEMINA FUPI NA MUBALIGHINA KUTOKA TANGA WILAYA YA LUSHOTO.


Bilal Muslim Mission hivi karibuni iliandaa Semina fupi iliyoshirikisha Mubalighina kutoka Tanga Wilaya ya Lushoto, Mubalighina hao wameushukuru uongozi wa Bilal Muslim Mission uliyopo Temeke jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha katika Sherehe ya Eid Al Ghadir pia Mubalighina hao walifurahi kuona namna taasisi ya Bilal inavyofanya Shughuli zake za Tabligh hasa katika upande wa Hawzat na Shule, Maulana Sayyid Arif amewataka Mubaligh hao kuandaa kikamilifu Majilisi ya Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imam Hussein (a.s) na kutoa ujumbe wa kweli katika jamii juu ya masahibu ya Imam (a.s) katika siku kumi za mwezi wa Muharram.