Ayatullah
Mohammed-Reza Mahdavi Kani Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu
Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Kusimamia
Kazi Zake amefariki dunia leo hapa mjini Tehran akiwa na umri wa miaka
84. Ayatullah Mahdavi Kani ameaga dunia leo baada ya kuugua kwa miezi
kadhaa kutokana na matatizo ya moyo aliyokuwa nayo ambapo alikuwa
amelazwa hospitalini tangu tarehe 4 Juni mwaka huu.
Ayatullah Mahdavi Kani mwanazuoni mtajika hapa nchini, alikuwa miongoni
mwa wanazuoni wanaharakati waliowahi kushika nyadhifa muhimu na nyeti
baada ya Mapinduzi ya Kiislamu hapa Iran. Marhumu Ayatullah Mahdavi Kani
aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia mwaka 1979-1981 katika
serikali ya Mashahidi Muhammad Ali Rajai na Muhammad-Javad Bahonar.
Aidha mwaka 1981 aliwahi kukaimu nafasi ya Waziri Mkuu. Katika kipindi
cha uhai wake, mbali na harakati zake za kisiasa, Ayatullah Mahdavi Kani
alikuwa akijishughulisha pia na kazi za kielimu ambapo alikuwa mhadhiri
wa Chuo Kikuu, Hawza na vile vile akialifu na kuandika vitabu. Viongozi
mbalimbali wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu wameendelea kutoa salamu za
rambirambi kufuatia kifo cha mwanazuoni huyo. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/ habari/iran/item/ 43898-ayatullah-mohammed-re za-mahdavi-kani-afariki-du nia
Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali
Khamenei ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Ayatullah
Mohammad-Reza Mahdavi Kani, Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu
Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika salamu
zake za rambi rambi kwa wananchi wa Iran, wanazuoni pamoja na familia ya
mwanachuoni huyo, Kiongozi Muadhamu amesema, Ayatullah
Mahdavi Kani alikuwa shujaa na sahibu wa kweli na mtiifu wa Imam
Khomeini RA. Ameongeza kuwa Ayatullah Mahdavi Kani alikuwa mkweli kama
mwanazuoni wa kidini, mwanasiasa na mwanamapinduzi. Aidha ameongeza kuwa
mwanazuoni huyo aliyeatangulia mbele ya Haki, hakuzingatia hata kidogo
masuala ya kimirengo au kikabila katika harakati zake. Ayatullah Mahdavi
Kani ameaga dunia leo akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa
miezi kadhaa kutokana na matatizo ya moyo ambapo alikuwa amelazwa
hospitalini tangu tarehe 4 Juni mwaka huu. Rais Hassan Rouhani pia
ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Ayatullah Mahdavi
Kani na kutangaza siku mbili za maombolezo rasmi nchini Iran. Chanzo cha
habari: http://kiswahili.irib.ir/ habari/kiongozi/item/ 43909-kiongozi-muadhamu-aom boleza-kifo-cha-ayatullah- kani