WITO KWA WAUMINI NA WATU WOTE.


"Ni bora sisi sote tufutike katika uso wa dunia tukakutane na Mola wetu aliyakuwa tuna amani kuliko kuwaacha Wahhabi (Answaru Sunna) waingilie miji yetu kwa kisingizio cha kusimamisha dola ya Kiislam na kuuwa watu wasio na hatiya." Uislamu haukuja kwa ajili ya kueneza mauaji dhidi ya wengine Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuja kwa ajili ya kueneza upendo na amani kwa watu wote, Uislamu walioshikamana nao watu hawa wanaojihita Answaru Sunna (Mawahhabi) wakumwaga damu za watu sijui wameupokea kutoka wapi? tunapenda kutoa wito kwa watu wote kuwa makini na watu hawa wanaolingania kuuwa kwa madai ya kusimamisha dola ya Kiislamu tambueni kuwa watu hawa sio Waislamu bali wamevaa vazi la Uislamu. "Tushikamane kupiga vita mauaji haya ya watu wasio na hatiya."