ATHARI MBAYA ZA UWAHABI NA HATARI ZAKE
Sehemu ya pili
Asalam alaikum wapenzi wasomaji wa makala yetu ya uwahabi,leo hii kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunakutana tena sote tukiwa wazima wa afya, ili kuelimishana madhara ya vijidudu hatari kwa afya zetu za kimwili na kiroho,vijidudu hivi hatari (mawahabi) hushambulia dini yetu huku vikijibatiza majina mazuri kama vile Answar Suna,Salafi Swaaleh,Ahlusuna wal jamaa,nk na kwa majina hayo wamewadanganya waislam wengi na kuwaingiza katika genge la wavaa kaptula au kanzu za watoto.
Katika sehemu ya kwanza ya makala hii tulisema kuwa : Tauhidi aliyoikusudiwa Muhamadi bin Abdul-wahab si tauhidi tauhidi ile tuijuayo waislam.
Sasa katika sehemu hii ya pili ya makala yetu,tutaelezea tauhidi kwa mtazomo wa sheikh Muhamad bin Abdul-wahab.
Anasema Mwanachuoni mashuhuri Mahmud Alusi katika kitabu chake:Taarikh Najdi,kama alivyonukuliwa na Sayyed Muhsin Al-amin “Alizaliwa Muhamad bin Abdul-wahab katika mji wa Uyainah huko Najdi ,na alisoma kwa baba yake fiq-hi kwa mujibu wa madhehebu ya Imam Ahamd bin Hanbal,na alikuwa tokea utotoni kwake akiongea maneno ambayo watu hawayafahamu,akiwapinga watu katika mengi ambayo ni sahihi kuyafanya kwa mujibu wa madhebu yao,na akawa shadidi katika swala la watu kuomba Mungu kupitia kaburi la bwana mtume Muhamad (s.a.w.w),kisha akaondoka kuelekea Najdi na baada ya hapo alikwenda Basra akikusudia kufika hadi Sham (Syria),na alipoingia Basra alibaki hapo muda tu na hapo alisoma kwa sheikh Muhamad Al-majmuui.
Hapo (Basra) aliwapinga watu katika imani aliyowakutanayo,basi wakamfukuza,naye akaondoka hapo kama mkimbizi,kisha baada ya kusumbuka sana akaingi katika mji wa Huraimalah,na baba yake alikuwepo mjini hapo,aliambatana na baba yake ,na akasoma tena kwa baba yake ,kisha akadhihirisha upinzani kwa waislam wa Najdi katika imani zao,baba yake alimkataza lakini hakukoma mpaka ukaibuka ugomvi baina yake na baba yake,na yakaibuka mabishano na marumbano mengi baina yake na waislam wa mjini hapo,basi akaishi hapo miaka miwili na mzee wake akawa amefariki Dunia mnamo mwaka 1153 H,na hapo sheikh akapata ujasiri wa kudhihirisha itikadi yake na kuwapinga waislam katika yale ambayo wao wameafikiana kuwa ni sahihi,Muhamad bin Abdul-wahab alipata wajinga wachache waliomuunga mkono,mpaka watu walipochoshwa na makala zake na kutaka kumuua ndipo alipokimbilia Uyainah ambako alikozaliwa.
Uyainah wakati huo ilikuwa ikongozwa na Othman bin Ahmad bin Muamar,baada ya kuwasili sheikh mjini hapo,alimtamanisha kiongozi Othman Muamar kuwa atamiliki Najdi nzima endapo atakubali kumsaidia na kumnusuru,Othman Muamar akamsaidia na wakafanya makubaliano kuwa mfalme atampa sheikh uhuru kamili wa kutangaza na kueneza itikadi zake,na sheikh atamsaidia mfalme kuitawala nchi nzima ya Najdi kwa njia yoyote ile,na ili kukomaza mahusiano yao Amir Othman alimuozesha dada yake Jawharah kwa sheikh Muhamad bin Abdul-wahab,sheikh akamwambia mfalme kuwa ni matumaini yangu kuwa Mungu atakuzawadia Najdi na vilivyomo .
Muungano baina ya wawili hao sheikh na mfalme haukudumu kwa kipindi kirefu,
Kwani sheikh aliwapinga waislam (kama kawaida yake),baadhi ya watu walimfuta,na akafanikiwa kuvunja kuba kwenye kaburi la Zaid bin Al-khatwaab.
Jambo hilo lilikuwa kubwa na habari ikamfikia Suleiman Al-hamiidi mfalme wa Ihsaa na Qatwiif,Suleiman alikuwa na nguvu zaidi ya Othman mfalme wa Uyainah basi akamuandikia barua Othman na kumuamuru amuue Muhamad bin Abdul-wahab,na akampa onyo ikiwa hata muua.
Othman akamwambia mgeni wake achague mji wa kukimbilia na sheikh akachagua kwenda DIr’iyah .
Othman akamteua bwana mmoja kwa jina Farid ili amsindikize sheikh Muhamad bin Abdul-wahab na kumuulia njiani,lakini bwana yule hakuweza kuumua bali alimuachilia aendezaka .
Sheikh aliingia DIr’iyah mnamo mwaka 1160H mji huo ulikuwa ukitawaliwa wakati huo na Muhamad bin Saud,na hapo pia akamshawishi Muhamad bin Saud kuwa atamuwezesha kuitawala Najdi nzima,mfalme alimuunga mkono na wakakubaliana kuanzisha vita dhidi ya waislam wote wanaokataa mtazamo wa sheikh na utawala wa Muhamad bin Saud,na hiyo ndiyo tauhidi iliyokusudiwa na sheikh Muhamad bin Abdul-wahab na yeyote anayekwenda kinyume na mawazo yake huyo ni mushriki na damu yake ni halali,basi mfalme akaamuru watu wa Dar’iyah kuingia katika jihadi ya kuuwa waislam nao wakamkubalia,mashambulizi yakaanza wakawapiga watu wa Najdi na Ihsaa mara nyingi tu,mpaka baadhi yao wakatii kwa lazima na uongozi wa Najdi nzima ukawa chini ya ukoo wa Saud kwa kutumia nguvu.
Mnamo mwaka 1207H alifariki sheikh Muhamad bin Abdul-wahab kisha baada yake akafa mfalme Muhamad bin Saud,na kumuacha mtoto wake Abdul-Aziz,naye alifanya kazi ya kuinusuru madhehebu na kupigana na kuuwa waislam kwaajili ya madhehebu ,kisha akafa Abdul-Aziz na kumuacha mwanawe Saud lakini Saud alikuwa shadidi mkali mno katika uwahabi zaidi ya baba yake ,Saud huyu aliwazuia waislam kwenda hija na akavuka mipaka katika kuwakufurisha wanao kwenda kinyume na wao,Saud naye alifariki na kumuacha mtoto wake Abdullah”. Taz Taarikh Najdi: uk 98-99.
Wapenzi wasomaji huu ndio uwahabi uliojengeka juu ya misingi ya matusi chuki,mauaji,dhulma,kukufurisha waislam ,utovu wa nidham kwa wazazi, kama alivyokuwa sheikh Muhamad bin Abdul-wahab akigombana na baba yake hali kadhalika na mashekih wake.
Na hayo ndiyo yanayojiri katika jamii yetu ya leo,waislam wasio na hatia wanauawa kwa anuani ya jihadi,majumba ya ibada yanayomilikiwa na watu wenye imani ghairi ya uislamu yanavunjwa na mawahabi,kumbukumbu na athari za dini hazitakiwi kwa mawahabi,ila kumbukumbu za wafalme wa kisaud ndizo zitakiwazo katika jamii za kiwahabi,yote hayo tutayazumnguza kwa mapana tukifikia mahala pake,ila nawaomba wapenzi wasomaji wajitahidi kadri ya uwezo wao,wapate nakala ya kitabu : Upotovu wa madhehebu ya uwahhabi.
Uwahabi ni genge la hujuma lililoasisiwa kwa lengo la kuidondosha dola ya Bani Hashim na kusimika utawala haramu wa kisaud.
Sheikh Ahmad bin Zaini Dahlaan,katika kitabu chake : Khulaasatul kalaam fi umarail balad alharam ameandika :”Hakika mawabi walipeleka wanazuoni wao 30 katika dola ya sharif Masud bin Said bin Zaid aliyefariki mwaka 1165H, basi sharifu akawaamuru wanazuoni wa Maka na Madina wafanyenao mjadala,basi wakajadiliana nao na kukuta itikadi zao ni mbovu,ndipo kadhi akatoa hukumu ya kuwakufurisha na akaamuru wafungwe,basi wakafungwa baadhi yao na wengine wakakimbia,dola ya masharif Masud,Ahmad,Ghalib na wengineo tutazizungumzia mahala pake.
Wapenzi wasomaji najua mtakuwa na shauku ya kupata jibu la swali namba 4 katika sehemu ya kwanza ya makala hii, swali lililohoji : Je, ni nani aliyepandikiza mbegu za madhehebu hii kwa mara ya kwanza ?
Jibu : Mbegu hizo zilipandikizwa mwishoni mwa karne ya saba na mmoja wa wanazuoni wa madhehebu ya Hanbali,aliyefahamika kwa jina :
Ahamad bin Abdul Halim al-maaruf Ibnu Taimiyyah Al harrani Al damashqi aliyezaliwa mnamo mwaka 661 H na kufariki mnamo mwaka 728H (sheikh huyu tutamchambua vizuri mahala pake)alikuwa mkiritimba katika madhehebu ya Hanbal,alifufua baadhi ya itikadi za madhehebu ya ahlul hadith,madhehebu hii inatumia hadithi zilizopokelewa na maswahaba katika kuthibitisha maswala ya kiteolojia(kiitikadi) na hawataki mijadala ya kiitikadi wala kutumia akili katika maswala hayo,Ibnu Taimiyyah alifufua baadhi ya mitazamo yao kama vile kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe nk,Ibnu Taimiyyah hakuishia hapo bali aliingiza katika itikadi za masheikh waliotangulia mambo ambayo hawakuyaacha katika vitabu vyao.
Kwenda kutembelea kaburi la bwana mtume (s.a.w.w)ikawa ni bid’aa na shirki kwake,kutabaruku na athari za mtume na watu wa nyumba ya utume pia kwake ilikuwa ni kinyume na mafundisho ya tauhidi.
Alirithi fikra za waheshimiwa waliomtangulia za kumvunjia heshima na kumchukia Imam Ali na kwa misingi hiyo akaunda harakati ya usalafi,lakini kimbunga kikali kilimshambulia toka kila sehemu,wanazuoni wakafanya kazi ya kubainisha upotovu wa madhehebu yake hiyo ya uzushi,na hawakuathirika na madhehebu hiyo ila wachache miongoni mwa wanafunzi wake kama vile Ibnul Kayyim Al jawziyyah( 691-751H) na baadhi ya wafuasi walikuwa Sham(Syria)na wengine wachache walikuwa Misri,kwa hiyo mti wa usalafi ukawa umekauka mapema mno lakini kwa muda maalum.Na mnamo karne ya kumi na mbili 12H aliibuka Muhamad bin abdul wahab na kuumwagilia tena maji mti wa usalafi na kuufufua kwa mara nyingine,na kufuata nyayo za Ibnu Taimiyyah.Taz bidaayatul maarifa uk 52-54.
Na kwa sababu hiyo tu, mawahabi wanamwita Muhamad bin Abdul wahab : Sheikh Al mujadid,yaani sheikh mfufuaji wa suna zilizokuwa zimetoweka.
Mpaka hapa tunaweza kusema kuwa : Uwahabi ni usalafi mambo leo…
Itaendelea. Na Sheikh Kabwe.