HISTORIA FUPI KUHUSU HIZBULLAH


HISTORIA FUPI KUHUSU HIZBULLAH,MUQAWAMAH WA LEBANON,MALENGO YA
KUASISIWA KWAKE.JE,UGAIDI NI MOJA YA MALENGO YA HIZBULLAH KAMA
WASEMAVYO MAADUI WA HAKI AU LA?!.JE,HIZBULLAH WALISHA KUMBWA NA
VITENDO VYA UGAIDI ?!.JE,KUNA DALILI ZOZOTE KWAMBA  HIZBULLAH
IMEFANIKIWA KATIKA MALENGO YAKE YA KUASISIWA KWAKE ?!
---------------------------------
KARIBU NDUGU MDAU KATIKA MAKALA HII MURWA UPATE UFAFANUZI WA YOTE HAYO
YALIYOASHIRIWA HAPO JUU.
Hizbollah ni kundi la Muqawamah linaloundwa na (Mashia) wafuasi wa
Ahlul-bait (a.s) wanaopatikana katika Jamii ya Lebanon.Kundi hili
MWANZONI KABISA LILIUNDWA NA  WANAHARAKATI WA KISHIA LAKINI KWA SASA
LINAWAJUMUISHA WAPIGANIA HAKI WOTE WA KIISLAAM WA LEBANON MASHIA KWA
MASUNII NA HATA WASIOKUWA WAASLAAM  WA NDANI YA LEBANON PIA NI MEMBERS
WA HIZBULLAH.
Kwa sasa MUQAWAMAH WA HIZBULLAH unaongozwa na Sayyid Hasan Nasrullah
ambapo ameshika jukumu la uongozi tangu mwaka 1992.Yeye ni Katibu mkuu
wa Tatu wa Hizbullah,ambapo mwaka huo wa  1992 ameshika rasmi jukumu
hilo baada ya utawala wa Israel kumuua KIGAIDI aliyekuwa Katibu mkuu
wa Hizbullah zama hizo Sayyid Abbas al-Musawi.Mauaji hayo ya KIGAIDI
yalitendwa tarehe 16 February,mwaka 1992.
-------------------------------------
Kwa muhtasari: Hivyo Hizbullah ni sehemu ya Jamii ya watu wa
Lebanon.Mashia nchini Lebanon,wanaunda asilimia 41 ya idadi mzima ya
watu wa Lebanon.Na wapo kwa wingi katika maeneo ya matatu ya Lebanon
ambayi ni:1-Kusini mwa Lebanon.2-Beirut na maeneo kadhaa
yanayoizunguka Beirut,na Kasakazini mwa Bonde la Beqaa.3-Pamoja na
Kanda ya Hirmil.
Nchi hii ya Lebanon ilikuwa ikikaliwa kwa mababu na ukoloni wa
Ufaransa ambapo ilijipatia uhuru wake mwaka 1943,ikiwa ni tarehe 22
Novemba.Mkoroni huyu ((Ufaransa)) aliamua kuondoa Majeshi yake ya
uvamizi nchini Lebanon,mwaka 1946.
--------------------------------
Jamii ya Mashia nchini Lebanon ilianza kuwa na nguvu miaka ya 1960s na
70s,ambapo mwaka 1960 Imam Musa Sadr alikuja nchini Lebanon na
akaongoza jamii ya Mashia katika mji wa Tyre.
Mwaka 1969 aliteuliwa rasmi kuwa mkuu wa kwanza wa Baraza kuu la
Kiislamu la Shia.Mwaka 1974 alianzisha "Harakati ya Wanyonywaji
wanyimwaji" ((Movement of the Deprived)) ili kuleta hali ya mbinyo kwa
serikali ya wakati huo ikiwa lengo kuu ni kuleta hali nzuri na bora ya
kiuchumi na kijamii kwa Mashia,wafuasi wa Ahlul-bait wa Mtume
(s.a.w.w).
--------------------------------

HIZBOLLAH ILIUNDWA MWAKA GANI NA KWA MALENGO GANI:
----------------------------------
Israel iliivamia mara kadhaa Lebanon kiadui na kiuonevu,na historia
imesajili kwamba mwaka 1978 katika Operesheni iliyoitwa:((Operation
Litani)).Kisha ikaivamia tena mwaka 1982 na uvamizi huo wa kijeshi
ulijulikana kama (Lebanon war) ambapo Utawala haram wa Israel ulidai
kuanzisha vita hiyo kwa lengo la kuondoa PLO,nchini Lebanon.Na PLO
maana yake: (Palestine Liberation Organization),kwa maana:((JUMUIA YA
UKOMBOZI YA PALESTINA)).Jumuia hii wakati huo ilikifanya kazi zake
ikiwa nchini Lebanon ikijaribu kuendesha harakati mbalimbali ili
kuzikomboa Ardhi za Palestina kutoka katika makucha ya Utawala haram
wa Israel.

Mapinduzi ya Kiislaam ya Jamhuri ya Kiislaam ya Iran ya mwaka
1979,yalileta athari kubwa sana n amuhimu nchini Lebanon ambapo
yalipandikiza moyo wa kujiamini kwa walebanon,wakawa na fikra ya
kuunda Muqawamah kwa ajili ya kujihamu wao,mali zao na nchi yao kwa
ujumla dhidi ya maadui wa Kizayuni.Vyanzo vingi ninaashiria kuwa
harakati hizo za kutaka kuwa na Muqawamah zilianza mapema mwaka 1982
na ilipofikia mwaka 1985 kikaundwa rasmi chombo cha kutetea haki za
walebano wanaoonenewa na kushambuliwa mara kwa mara na utawala haramu
wa Isarel ambao wakati huo ulikuwa ukizikalia kwa mabavu ardhi za
walebanon ambapo ulionyesha kutokuwa tayari kurudisha ardhi hizo kwa
walebanon.

VYANZO RASMI VINASEMA:Hizbullah iliundwa na wafuasi wa Ragheb
Harb,Kiongozi wa Muqawamah wa Mashia wa upande wa Kusini mwa Lebanon
ambaye aliuliwa n autwawala wa Israel mnamo mwaka 1984 mwaka mmoja
kabla ya kuazishwa Hizbullah.
Kwa ufupi fikra na harakati za kuundwa kwa Hizbullah hazikuwa ispokuwa
kutokana na uvamizi wa Israel nchini Lebanon mbapo ukaliaji wa mabavu
wa ardhi za walebanon,uliwafanya walebanon kuwa na fikra pana nijinsi
gani wataweza kumuondoa adui aliyewavamia na kuzikalia ardhi zao
kimabavu.Na hapo ndipo Wana fikra wa Kiislaam wa lebanon,maadui wa
uvamizi na dhulma walipiunda unda chombo hiki kinachoitwa Kundi la
Mwenyeezi Mungu (Hizbullah) ili kurudisha heshima ya Taifa lao la
Lebanon na kumtimua adui vamizi.Kundi hili la Muqawamah lilipoundwa au
lilipoanzishwa lilipata uungaji mkono kutoka sehemu mbalimbali zenye
kupinga vita na uvamizi wa nchi fulani kwa nchi nnyingine.

Jamhuri ya Kiislaam ya Iran ndilo Taifa pekee la Kiislaam lililotoa
mchango mkubwa wa kifkra na uungaji mkono wa kimaada na kimaanawi kwa
wanaharakati hao wa Hizbollah wanaopigania uhuru na heshima ya
walebanon na Taifa zima la  Lebanon.
Hizbollah iliyoanza na idadi ndogo ya wanamapambano na wapigania haki
wa Lebanon,sasa hivi imekuwa ni Jumuia kubwa mno ikiwa na viti kadhaa
vya wabunge katika Serikali ya Lebabon,wakiwa na Redio Kituo cha
Televisheni,huku wakiwa na mipango kadhaa ya maendeleo ya Kijamii.
Jumuia hii ya Hizbullah kwa sasa ni Jumuia muhimu ndani ya Serikali ya
Lebanon,na inapata sapoti kubwa sana kutoka kwa Jamii ya Mashia wa
Lebanon,na imekuwa ni Jumuia yenye uwezo mkubwa wa kuitisha na
kuhamasisha maandamano ya Mamia na Maelfu nchini Lebanon dhidi ya
Utawala Haram wa Israel.

Hivyo,Hizbollah mbali na kuwa Muqawamah wa kutetea haki za walebanon
na kuweka huru ardhi zao zinazokaliwa na wazayuni,pia ni moja wapo ya
vyama vya Kisiasa nchini Lebanon vinavyoshiriki katika Serikali huru
ya Lebanon.
---------------------
HIZBOLLAH NI KUNDI LA KIGAIDI AU LA?!.
Tumeelezea wazi malengo ya kuundwa kwa Hizbollah,hivyo si kundi la
kigaidi kama makundi mengine yalivyo ya Kigaidi,bali ni wanaharakati
na wanamuqawah wa Lebanon,ambao lengo lao kuu ni kuhakikisha wananchi
wa Lebanon wanaishi kwa uhuru na amani pasina kubughudhiwa na wavamizi
wa Kizayuni,na harakati zao zimeonekana katika ya hivi karibu (Vita ya
mwaka 2006 na mwaka 2008) iliyoanzishwa na Israel dhidi ya Hizbullah
ambapo Hizbullah imeweza kuhakikisha malengo yake ya kuasisiwa kwake
kwa kurudisha ardhi za kusini mwa Lebanon zilizokuwa zimekariwa kwa
mabavu na utawala ghasibu wa Israel.Na huo ulikuwa ni ushindi mkubwa
uliopelekea utawalaha haram wa Israel kuhaha na kulaumiana wao kwa wao
kunatokana na kichapo walichokipata kutoka wanamuqawamah hao wa
Hizbollah.
Ndio,kwa Isarael na kwa maadui wa Kiislaam wa Kiislaam Hizbollah kwao
litakuw ani kundi la Kigaidi maana linapigana dhidi ya Israel na
kuteteta haki za ndugu zao wa wapalestina,wanaodhulumiwa na ardhi zao
kukaliwa kwa mabavu na Utawala haram na Ghasibu wa Israel.Hiyo ni
kawaida kwa adui maana siku zote gaidi hajioni kama ni gaidi pindi
afanyapo ugaidi,Isarel inafanya ugaidi si lebanon tu bali hata ndaniya
Jamhuri ya Kiislaam ya Iran kwa kuua Maulamaa wa Nyuklia wa
Iran,lakini hatujasikia ISRAEL ikisema mimi ni Gaidi au Marekani
ikisema:Israel ni kundi la kigaidi,ama wale wanaotoka na kujitetea
dhdi ya ugadi wa Israel ni kosa kubwa wanafanya kwa mtazamo wa wa watu
hao wenye kudai kuiongoza dunia (masuper power wa dunia),kwa
mantikihiyo Hizbollah inatakiwa kukaa kimya na kuiachia Israel itawale
itakavyo ardhi zao na kuikandamiza haki ya PALESTINA NA LEBANON,ama
wakitoka kuonyesha upinzani na kupigana kw akujihami dhidi ya maadui
wa Taifa lao,basi zinakuja fikra za kwamba HIZBULLAH NI KUNDI LA
KIGAIDI!!.VIPI MNAHUKUMU IKIWA KWELI NYINYI WAADILIFU?!.
------------------
HIZBOLLAH IMEKUMBWA NA UGAIDI,KUN AUSHAHIDI WOWOT EKUHUSU HILO?!.
------------------
Hizbullah ni moja ya watu waliokumba sana na ugaidi,mauaji ya hapa na
pale ya kigaidi yanayotekelezwa na utawala haram wa Isarel yamekuwa ni
mwiba kwa wanamuqawamah hawa wa Lebanon.Viongozi wengi wa Hzibollah
wameuliwa kigaidi na utawala huu haram wa Israel,kuanzia mwasisi wa
Hizbollah na wengine wengi.

Hivi karibu Israel imekiri wazi kumuua Kamanda Mughniya wa
Hizbullah.Habari zinasema: Balozi wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa
Israel nchini Ujerumani amekiri kwamba Shirika la Kijasusi la Israel
MOSSAD ndilo lililopanga na kutekeleza njama za kumuua Emad Mughniya
kamanda wa Hizbullah Februari mwaka 2008 mjini Damascus,Syria.Avi
Primor ameyaeleza hayo kwenye mahojiano na kanali moja ya televisheni
nchini Ujerumani na kusisitiza kwamba, utawala wa Israel ndio
uliotekeleza shambulio la kumuua kigaidi kamanda Mughniya.Hayo
yanajiri katika hali  ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel daima
umekuwa ukikanusha kumuua Mughniya au kuhusika katika kupanga njama za
kutekeleza shambulio hilo la kigaidi.Yote hayo yanafanyoka na kuonwa
na wanadunia,lakini hatujasikia hao wenye kuihami Israel wakisema
chochote kunako ugaidi wa Utawala huo wa Israel.Twende Palestina:Huko
nako Utawala huu umetekeleza  mashambulizi kadhaa ya kigaidi dhidi ya
viongozi wa Palestina na wapalestina,lakini tunalolisikia kutoka kwa
wenye kuuhami utawala Ghasibu wa Israel ni hili kwamba:Muqawamah wa
Palestina (HAMAS) ni kundi la kigaidi!!! kwa kuwa unaonyesha
resistance na muqawamah dhidi ya Mayahudi wa Kizayuni wanaozikalia kwa
mabavu ardhi zao.Basi ni nani gaidi na ni ipi maana sahihi ya Ugaidi
ikiwa Israel sio Taifa la Kigaidi?!!.Je,kutetea haki zako na kuihami
nchi yako na wananchi wa nchi yako ni ugaidi?!!.Mna nini nyinyi vipi
mnahukumu?!!.

La kushangaza na kusikitisha ni kusikia baadhi ya waislaam tena wenye
kudai wamesoma elimu safi ya dini ya Kiislaam wakidai kwamba:TUACHE
KUITANGAZA AU KUZUNGUMZIA CHOCHOTE KUHUSIANA NA HIZBOLLAH MAANA
MAREKANI IMESEMA NI KUNDI LA KIGAIDI?!!.Ni ajabu sana kusikia kauli
kama hizo kwa watu ambao wengi tunatarajia kuwa wana akili na wamesoma
na kuelimika,lakini inasikitisha kuona wamebeba nembo ya elimu katika
jamii zetu kisha wanatoka na fikra za kwamba Marekani kaisha sema
Hizbullah ni kundi la Kigaidi hivyo tuache kuzungumzia chochote
kuhusiana na Hizbollah ati huenda Serikali ikamchukulia hatua mwenye
kuizungumzia Hizbullah!!!
-----------
Binafsi nimekutana na watu hao wakibeba fikra hizo,sikutumia muda
wangu kuwashangaa niliposikia wakizunguza fikra kama hizo
zilizooza,ispokuwa nilichokifanya niliutumia muda wangu kuwauliza
maswali kadhaa kama ifutavyo;
Niliwauliza hivi:Marekani ipo wazi kwamba ni maadui wa uislaam,hivyo
ikitokea siku wakasema hatutaki kuona waislaam wakiswali,ina maana pia
mtasema kuwa tuache kuswali maana Marekani yuko dhidi ya swala na
kaisha  onyesha upinzani wake dhidi ya hilo?!.Au ikitokea Marekani
akasema:Uislaam ni ugaidi(na kaisha sema kuhusu hilo!!) je,ni sahihi
kwamba tuache kutangaza uislaam wetu wala kufanya Tabligh wazi wazi
kwa kuwa Marekani kasema UISLAM NI UGAIDI?!.Mpak aleo sijapara majibu
ya maswali hayo.Kuna watu wengine wamelewa umarekani na Marekani kwako
ni Mungu wa Pili.Allah (s.w) atuepushe na watu hao wenye kujijua haki
kupitia mtazamo wa Marekani na Magharibi.

Mwandishi wa Makala hii: Tzchalii.