Semina ya kujenga umoja na mshikamano baina ya
Waislamu na dini zote za mbinguni imefanyika usiku huu wa tarehe
18/06/2014 mjini Posta,jijini Dar es Salaam, Katika Semina hiyo viongozi
wa kidini wametakiwa kutoa elimu katika jamii kutokana na matukio
yanayoendelea hivi sasa ulimwenguni, viongozi hao wametakiwa kufichua
njama dhidi ya makundi haramu yaliyojivisha sura ya Uislamu.