Sheikh Abdullatif Swaleh ametembelea Mkoa wa
Tanga, Wilaya ya Lushoto katika msafara wake amebahatika kukutana na
Mwanaharakati mkongwe Sheik Waziry Nyello aliyekuwa Mwenyekiti wa
Tanzania Ithna Asharyyah Community (T.I.C) yenye makazi yake
Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Sheikh Waziry kipindi cha uongozi
wake katika taasisi hiyo alisimama kidete kutetea haki za wanyonge na
kusimamia maendeleo ya vijana hasa katika upande wa elimu pia alipinga
kila aina ya ubaguzi dhidi ya mtu mweusi, alikemea manyanyaso dhidi ya
wanyonge kwa wenye nacho katu hakusita kumfuata mtu pindi anapokosea kwa
kweli hatuna budi kufuata nyayo zake, Sheikh Abdullatif amesema wilaya
ya Lushoto bado ipo nyuma sana kiharakati inaitajika viongozi wake
watembelewe mara kwa mara kwa ajili ya kuwatia nguvu ya ufanyaji kazi
kwani viongozi hao wamekuwa na malalamiko ya mara kwa mara ya kutopewa
ushirikiano baina yao na taasisi nyingine.