Rais
Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufuatwa
njia na nyayo za Imam Khomeini MA ni fahari kubwa kwa Waislamu.
Akihutubia hadhara ya wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wanaokuja
kushiriki maadhimisho ya kutimia 25 ya kufariki dunia Imam Khomeini,
Rais Rouhani ameongeza kuwa, Imam alianzisha harakati kubwa ya Kiislamu
yapata miaka 50 iliyopita. Rais Rouhani ameongeza
kuwa, hakuna mtu yeyote aliyefikiri na kutasawari kwamba katika kipindi
kifupi tu Imam angeliweza kukabiliana na matatizo yote ya ndani na
kimataifa na hatimaye kujipatia ushindi adhimu. Rais wa Iran amesema
kuwa, katika kipindi cha miongo mitano iliyopita, Iran ilikuwa chini ya
ukandamizaji wa madola ya kibeberu na kusisitiza kwamba wananchi wa Iran
wenye uzoefu wa ustaarabu wa maelfu ya miaka waliupokea Uislamu baada
ya kubaathiwa na kupewa utume Mtume Muhammad SAW. Ameongeza kuwa, Iran
ilikuwa na nafasi muhimu katika ustawi wa utamaduni na ustaarabu wa
Kiislamu, lakini inasikitisha kuona kwamba katika karne za hivi karibuni
haikuwa na nafasi yoyote kiutawala. Rais Rouhani ameongeza kuwa, madola
ya kibeberu na hasa Uingereza na Marekani yalikuwa yakiingilia masuala
ya ndani ya Iran na katika masuala muhimu na nyeti ya kitaifa hapa
nchini, na kuyatolea maamuzi bila ya ridhaa ya wananchi, lakini Imam
Khomeini alisimama kidete na kukabiliana na madola hayo ya kibeberu
duniani. Imeelezwa kuwa, jumla ya shakhsia 400 wa kiutamaduni, kidini ,
kisiasa na wahadhiri kutoka nchi 29 duniani wapo nchini kwa lengo la
kushiriki kwenye maadhimisho hayo.
Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa: kushikamana na Qur'ani
ni jambo ambalo litauletea Umma wa Kiislamu heshima.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo Jumanne hapa mjini Tehran wakati alipokutana na mjumuiko wa maustadhi, maqarii na mahufadh walioshiriki katika Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu. Ameongeza kuwa, lengo la juu la kuihifadhi na kuisoma Qur'ani Tukufu ni 'kufahamu na kutekeleza' maamrisho yake sambamba na 'kufungamana na maneno ya Mwenyezi Mungu. Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa: "Uongofu wa Mwenyezi Mungu" na "Kufahamu vigezo vya kimsingi vya Qur'ani katika masuala muhimu kama vile kumfahamu ipasavyo adui" ni kati ya nukta muhimu za kufungamana na Qur'ani.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema tatizo kubwa zaidi la ulimwengu wa Kiislamu ni kujiweka mbali na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na natija ya hilo imekuwa ni kughafilika Waislamu kuhusu njama na ukhabithi wa maadui wa Uislamu. Ameongeza kuwa njia ya kufidia upungufu huu wa kimsingi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kufahamu kwa kina vigezo vilivyowekwa katika Qur'ani Tukufu. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, sera za maadui wa Uislamu zimejengeka katika msingi wa kuzusha vita vya ndani kupitia vibaraka na kusababisha ndugu wauane wao kwa wao katika jamii za Kiislamu. Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kuna baadhi ya watu katika Umma wa Kiislamu hawafahamu hizi sera sumu za maadui bali hata wako tayari kumpa shetani mkono na kushirikiana na hata utawala wa Kizayuni wa Israel katika kukabiliana na ndugu zao Waislamu.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, maadui wa Uislamu walizidisha njama zao dhidi ya Uislamu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria namna vijana wa Iran walivyoikumbatia kwa wingi Qur'ani Tukufu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema, hiyo ni neema kubwa. Ameongeza kuwa, kufungamana na Qur'ani kunaikaribisha jamii katika mafundisho yaliyojaa uhai ya kitabu hicho kitukufu na kwamba hilo ndilo lengo kuu na la juu katika kuhifadhi na kuisoma Qur'ani Tukufu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kusema kuwa: "Kwa kufungamana na Qur'ani, umma wa Kiislamu unaweza kuelekea katika izza ambayo Mwenyezi Mungu SWT amewaahidi."
Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalimalizika jana hapa Tehran baada kufanyika kwa muda wa wiki moja. Mashindano hayo yalianza tarehe 27 Rajab katika mkesha wa maadhimisho ya kubaathiwa Mtume Muhammad SAW. Mashindano hayo yalikuwa na maqarii na mahufadh 120 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 75 duniani huku kukiwa na jopo la majaji 15 ambapo 10 kati yao ni kutoka nchi za kigeni na watano ni Wairani.