Kumbukumbu
ya kifo cha Imam Khomein (R.A) imefanyika leo katika ukumbi wa Jafarry
Complex,jijini Dar es Salaam, karibu na jengo la umoja wavija wa CCM.
Imam Khomeini katika uhai wake hakuwahi hata sekunde moja kupuuza jambo
lolote katika mikakati ya kuinua jamii
ya Kiislamu, hivyo alikuwa Kiongozi wa kisiasa mwenye changamoto na
harakati nyingi ulimwenguni. Imam alifariki mnamo tarehe 3/06/1989 usiku
siku ya Jumamosi. Imam alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo, sababu
iliyopelekea kifo chake ni ugonjwa uliyopatikana kwenye mfumo wa chakula
hivyo alilazimika kufanyiwa upasuaji. Imam Khomein wakati wa uhai wake
aliamini dharura ya kuwepo mipango, ratiba na udhibiti wa nafsi katika
maisha, hivyo alikuwa akitenga muda maalumu usiku na mchana kwa ajili ya
ibada, dua, na kisomo cha Qur'an. Alikuwa akishiriki mazoezi ya
kutembea huku akimtaja Mwenyezi Mungu na kufikiria mustakbali, kiasi
kwamba alifanya kufikiria mustakbali ni sehemu ya ratiba yake ya kila
siku. Pamoja na kuwa na kazi nyingi na mikutano ya mara kwa mara na
viongozi wa utawala wa Kiislamu lakini suala la kukutana na watu wa
kawaida alilipa umuhimu wa pekee, hivyo aliendelea na ratiba yake ya
kila wiki ya kukutana na familia za mashahidi hadi siku za mwisho za
maisha yake. "KUMUENZI IMAM KHOMEIN NI KUFUATA NJIA YAKE."