Sheikh Ilunga amefariki dunia kwa ugonjwa wa kisukari jijini Dar es Salaam. Mwili wake umeswaliwa Msikiti wa Kichangani, Magomeni – Mapipa jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika Makaburi ya Mwinyi Mkuu hapo hapo Magomeni. Sheikh Ilunga alikuwa Muhadhiri wa Kiislam nchini Tanzania na Afrika Mashariki, aliwahi kukamatwa na Polisi na kufunguliwa mashitaka mwaka jana akiwa na viongozi mbalimbali wa dini, wakituhumiwa kwa kosa la uchochezi wa dini kupitia CD na DVD wanazoziuza kwa waumini wa dini ya Kiislam zinazoeneza chuki. "Hakika sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea."