Mitume wa Mwenyezi Mungu wakiongozwa na Mtume Muhammad (S.A.W.W) na Ahlul Bayt wake watoharifu ndio walio katika daraja ya juu zaidi kwa mtazamo wa kuwaongoza wanaadamu. Baada yao maulamaa na wanazuoni Waislam ndio waliorithi jukumu la kueneza risala ya Mwenyezi Mungu.