Taasisi
ya Bilal Muslim Mission imeandaa Semina fupi ya siku mbili kwa
Mubalighina wanaofanya kazi ya kueneza mafundisho sahihi ya Uislam wa
Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) Semina hiyo imeanza siku ya J.nne ya
tarehe 06/05/2014 Bilal Temeke, jijini
Dar es Salaam, katika Semina hiyo wameshiriki Masheikh na Walimu wa dini
kutoka sehemu mbalimbali Lushoto,Rufiji Ikwiriri, Kondoa, Mtwara
Arusha, Moshi, n.k katika Semina hiyo wameudhuria takribani watu 40
Semina inatarajia kumalizika siku ya Jumatano tarehe 07/05/2014.