Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Marekani imekasirishwa na hatua ya taifa la Iran ya kusimama kidete mbele ya mgawanyiko wa dunia katika kambi ya mabeberu na wanaojisalimisha mbele ya mabeberu.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran wakati akihutubu katika mahafali ya kuhitimu maafisa wa kijeshi katika Chuo Kikuu cha Kijeshi cha Imam Hussein AS. Ameongeza kuwa madola yenye kiburi yamekasirishwa sana na ustawi wa taifa la Iran na kuongeza kuwa, "nasi katika kuwajibu tunakariri kauli maarufu ya Shahid Beheshti ambaye alisema 'kufeni na hasira zenu'."
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hatua ya madola ya kibeberu ya kuibua maudhui kama vile nyuklia, haki za binaadmau na masuala mengine dhidi ya Iran ni kisingizio tu kwani lengo lao ni kutumia visingizio hivyo kulishinikiza taifa la Iran ili liache kusimama kidete mbele ya mfumo wa kibeberu duniani. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa taifa la Iran kamwe halitasalimu amri mbele ya mabeberu hao. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa taifa la Iran limeweza kuthibitisha uwezo wake katika medani mbali mbali na limefanikiwa kuonyesha kuwa bila kuitegemea Marekani limepata ustawi mkubwa wa kisayansi, kijamii sambamba na kuwa na ushawishi wa kimataifa na izza ya kisiasa. Ameashiria njama za vyombo vya habari vya mfumo wa kibeberu duniani ambavyo vimekuwa vikijaribu kuwazuia walimwengu kupata habari sahihi kuhusu ustawi na mafanikio ya taifa la Iran na kusema kuwa pamoja na kuwepo njama hizo, leo idadi kubwa ya watu wa dunia wanaliamini taifa la Iran na kwamba waliowengi duniani wako na taifa la Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa utumizi wa ibara yenye kuhadaa ya 'Jamii ya Kimataifa' wakati wa kukabiliana na Iran na kusema, ukweli wa mambo ni kuwa, hayo madola ya kibeberu si jamii ya kimataifa bali ni nchi chache tu zenye kiburi ambazo ziko chini ya usimamizi wa mashirika yanayofungamana na Uzayuni. Ayatullahil Udhma Khamenei amesema, jamii ya kimataifa ni mataifa na serikali zinazodhulumiwa ambazo kutokana na mashinikizo ya madola ya kibeberu hazithubutu kupinga madola hayo yanayotumia mabavu. Amesema iwapo mazingira yatajitokeza, nchi zinazodhulumiwa bila shaka zitatangaza bayana upinzani wao kwa madola ya kibeberu. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Uislamu ndio njia pekee ya kumuokoa mwanaadamu kutokana na maafa mbali mbali ambayo yamekuwa yakijiri kwa karne kadhaa sasa. Ameongeza kuwa Uislamu ndio njia pekee ya kumletea mwanaadmau heshima ya kweli. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, vijana waumini ndio wajenzi wa Iran ya baadaye na kwamba ndio chanzo cha kuibuka 'ustaarabu mpya wa Kiislamu'. Chanzo cha habari (irib)
Someni
hadithi za Mtume (s.a.w.w) zilizokusanywa na Ahlul-Bayt (a.s) ndio
mtajua Mtume(s.a.w.w) alikuwa wanamna gani?, matatizo yote haya
yanayotokea ulimwenguni mtayaona Mtume (s.aw.w) ameyasema na ufumbuzi
wake ameusema leo utasitaajabu kuona mtu
kama Imam Khomein ameweza kupambana na Mmarekani ni kwa sababu
amezisoma hadithi za Mtume (s.a.w.w) ambazo zilizuiwa zisitolewe na
baadhi ya Masahaba, leo hii Waislam mnaogopa kuzishika hadithi hizo na
mkipewa kitabu cha hadithi zilizopokewa na Ahlul-Bayt (a.s) mnazificha
kwa kuhofia kuonekana nazo na matokeo yake mnasoma hadithi za watu ambao
wamelaniwa na Mtume (s.a.w.w).