WATAFITI WA MAMBO YA KALE WAMETEMBELEA TAASISI YA AL-ITRAH FOUNDATION.

Wataalamu wa historia ya mambo ya kale wenye taasisi yao nchini Iran wametembelea taasisi ya Al-Itrah Foundation yenye makazi yake Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia jinsi gani wataweza kufanya kazi ya kutafsiri kazi zao kwa lugha ya Kiswahili ili waweze kufikisha hujumbe mbalimbali juu ya historia katika jamii ya Kitanzania.