Imepokewa kwamba mtu alimwambia Imam Husein (as): “Kaa ili tujadiliane
katika dini.” Akasema: “Ewe mtu, mimi najua dini yangu na najua uongofu
wangu, kama wewe hujui dini yako basi nenda ukaitafute, ni wapi mimi na
majadiliano!! Hakika shetani anamshawishi mtu na anamnong'oneza na
kumwambia: Jadiliana na watu katika dini ili watu wasihisi mapungufu
yako na ujahili wako."Rejea: Biharul- An’war, Juz. 2, Uk.135 Hadith 32.
Na hili nisomo kubwa, na ni wajibu tulitafakari, hakika mwanadamu inapasa asivutike kwenye mjadala usio natija. Napenda kutoa angalizo kwamba maneno haya ya kiubaguzi ya kimadhehebu ambayo yamejaa anga yanataka kushughulisha watu na mijadala tasa.Nasaha yangu kwanafsi yangu na kwa ndugu zangu wananchi wote ni kwamba wajiepushe kuingia katika mjadala huu. Wakati mwingine unaona katika madrasa au chuo kikuu au katika sehemu yoyote mjadala unaotokana na yale wanayoyasikia katika runinga, na baadhi wanadhani kwamba ni wajibu wake kujitetea, na kama hajajadili atakuwa dhaifu, na kutokana na mantiki hii baadhi wanatumbukia na kuvutika katika mjadala huu tasa, ambao haujulikani utaishia wapi. Asidhani yeyote kwamba kwa kujibu kwake anatumikia madhehebu na itikadi, dhana hii ni makosa.
Na mara nyingi lengo la upande mwingine la mjadala ni uchochezi na kutengeneza tatizo,tumeshuhudia na tumesikia mengi katika nyanja hii, na kwa sababu hii Qur'an inawasifu waumini kwa kauli yake (swt): “Na wale ambao hawawi kwenye uzushi, na wanapopita kwenye upuzi hupita kwa heshima zao.” (Surat Furqan: 72). Pia Mwenyezi Mungu anasema: "Na waja wa Mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu. Na wajinga wakiwasemesha, husema: 'Salama.'" (SuratFurqan:63).
Kama tungesoma vitabu vya Hadithi kama vile al-Kafiy na Biharul-An’war tungekuta riwaya nyingi kutoka kwa Maimamu wetu (a.s) kuhusu majadiliano, mazungumzo na kujionyesha katika dini, nazo ni hadithi zinazokataza hali hiyo, Imam as-Sadiq (a.s) anasema: "Jihadharini na ugomvi katika dini hakika unazizuia nyoyo kujishughulishana utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu." Rejea: Biharul- An’war, Juz. 2, Uk.128 hadith 6. Na nasema: “Msigombane na watu kwa ajili ya dini yenu hakika ugomvi unaleta ugonjwa katika nyoyo, waacheni watu hakika watu wamechukua kutoka kwa watu." Rejea: Biharul- An’war, Juz. 2, Uk.133 hadith 24.
Na ni wazi kwamba wewe huwezi kubadilisha ukinaikaji wa wengine; kwa sababu wao wamechukua maarifa yao kutoka kwa masheikhe wao wanaowazingatia kuwa ni watukufu na wanawaheshimu. Na kuna riwaya kutoka kwa Imamu al-Baqir (as) ambayo inatia mkazo juu ya dharura ya kuwa mbali na mjadala na majadiliano tasa, inawaeleza Mashia kwa sifa ya ajabu, Imam anasema: "Hakika Mashia wetu hawazungumzi." Rejea: Biharul- An’war, Juz. 2, Uk.135 hadith 33. Ikimaanisha kujiepusha kwao na hali hii isiyo nafaida.
Hadi mmoja wa wanafunzi wa Imam as-Sadiq (as) alimwambia Imam: “Imenifikia kwamba wewe umechukia kujadiliana na watu.” Akasema: "Ama maneno ya aliye mfano wako hayachukiwi, ambaye akiruka anajua kutua vizuri bila kuanguka, na akitua anajua kuruka vizuri, ambaye yuko hivi hatumchukii." Rejea: Biharul- An’war, Juz. 2, Uk.136 hadith 39 Na amesema Abdul-Ulaa: Nilimwambia Abu Ja'far: “Hakika watu wanamtia dosari Ali kwa maneno, na mimi najadiliana nao.” Akasema: Ama mfano wako,ambayeanatua kisha anaruka, huyu ni bora, ama anayetualakini hawezi kuruka, huyu hapana." Rejea: Biharul- An’war, Juz. 2, Uk.136 hadith 38
Hapa tunatia mkazo kwamba mtu yeyote ambaye ana uwezo wa kutatua mambo kwa njia sahihi inasihi kwake kujadili, ama ikiwa hawezi hayo kama ikiwamaarifa yake ni madogo au hawezi kudhibiti hasira zake basi mjadala sio katika maslahi yake na madhehebu hayanusiriwi kwa mjadala bali yananusurika kwa amali njema.